Kitaifa

MAAFISA KAZI NCHINI WATAKIWA KUTOA ELIMU YA SHERIA ZA KAZI

Written by mzalendo

Na. Mwandishi wetu, Dar es salaam

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na wenye ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja amewataka Maafisa kazi Wafawidhi nchini kutembelea maeneo ya kazi ili kubaini migogoro iliyopo na kutoa elimu ya sheria za kazi.

Mhandisi Luhemeja amebainisha hayo Desemba 20, 2023 Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifanyiwa mahojiano kupitia kipindi cha Mizani kinachorusha kila alhamisi kupitia TBC ambapo alihojiwa kuhusu Mageuzi yenye Tija katika Sekta ya Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu.

Amesema mbali na jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, katika uwekezaji kumekua na changamoto ya migogoro baina ya wananchi na wawekezaji inayochochewa na kutokufahamu sheria za kazi.

Vilevile, amesema kushidwa kutafsiri sheria za kazi kati ya wafanyakazi na mwajiri kunapelekea migogoro inayokwamisha shughuli za kiuwekezaji na kutengeneza uhasama baina ya wananchi na wawekezaji.

About the author

mzalendo