Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Afisa Mitihani kutoka Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Bi. Fatma Muhidini Mshana kuhusu utengenezaji wa Vyeti pamoja na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Baraza hilo wakati wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) katika Ofisi za Baraza hilo Jijini Dar es Salaam
…………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kushirikiana na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuendelea kufunga mtandao katika vijiji vyenye umeme ili kuwawezesha wanafunzi kufanya mitihani ya masomo ya sayansi kwa mtandao.
Rais Samia ametoa maagizo hayo leo wakati wa hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) iliyofanyika katika Ofisi za Baraza hilo.
Aidha, Rais Samia amesema serikali imefanya uwekezaji kwenye TEHAMA ambao umeimarisha utendaji wa Baraza na kuongeza matumizi ya teknolojia katika usajili wa watahiniwa, uchapaji na usahihishaji wa mitihani na uchakataji wa matokeo.
Rais Samia pia amesema Serikali itaendelea kuijengea uwezo NECTA na walimu ili kuhakikisha ufundishaji, usomeshaji na utahini unafanyika kwa umahiri mkubwa kuwawezesha watahiniwa kumudu mahitaji ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Vile vile, Rais Samia ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na NECTA kutafuta mkakati wa kushughulikia changamoto ya udanganyifu wa mitihani.
Aidha, Rais Samia pia amelitaka Baraza la Mitihani kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kuendana na shabaha ya sera ya elimu hususan katika upimaji wa umahiri.
Rais Samia amesema serikali itaendelea kuimarisha utendaji wa Baraza kulingana na mazingira mapya ya kiteknolojia na kushirikiana na Baraza hilo ili lifikie malengo ya muda mrefu ya kuweka mitambo ya kisasa ya uchapaji kadri uwezo utakavyoruhusu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda kuzindua mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwenye hafla iliyofanyika katika Ofisi za Baraza hilo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kibao cha Uzinduzi wa mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwenye hafla iliyofanyika katika Ofisi za Baraza hilo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Afisa Mitihani kutoka Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Bi. Fatma Muhidini Mshana kuhusu utengenezaji wa Vyeti pamoja na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Baraza hilo wakati wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) katika Ofisi za Baraza hilo Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasikiliza Watoto wa Shule ya Msingi Kisutu wakati wakitumbuiza mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2023.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika Ofisi za Baraza hilo Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2023.
Viongozi wa Dini wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika Ofisi za Baraza hilo Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika Ofisi za Baraza hilo Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2023.
Baadhi ya Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika Ofisi za Baraza hilo Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi wa Chapa na Uchapishaji kutoka Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Edward Haule kuhusu shughuli mbalimbali za uchapaji wa Mitihani pamoja na Nyaraka mbalimbali wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza hilo Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2023.