Uncategorized

MHE. KIKWETE:MIFUMO MIPYA YA UTENDAJI KAZI SERIKALINI KUWABANA WATUMISHI WASIOFANYA KAZI

Written by mzalendo
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza  leo na Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha ( ATC) ikiwa ni muendelezo wa ziara  yake ya kukagua maendeleo ya mafunzo ya mfumo wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma kutika Chuo  Ufundi Arusha ( ATC)  yaliyofanyika katika Chuoni hicho 
Mkurugenzi wa Maadili kutoka Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora  ambaye pia ni Mwezeshaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Utendaji Kazi kwa Watumisgi wa Umma ,Bi. Leila Mavika  akizungumza kabla ya kumkaribisha  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe.Ridhiwani Kikwete 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa ameongozana na Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha( ATC)  Dkt.Musa Chacha wakati akitembelea Chuo hicho  mara baada ya kukagua maendeleo ya mafunzo ya mfumo kwa watumishi wa umma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na baadhi ya wanafunzi wakati akitembelea Chuo cha Ufundi Arusha ( ATC)  mara baada ya kukagua maendeleo ya mafunzo ya mfumo kwa watumishi wa umma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na baadhi ya timu ya na Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha ( ATC) pamoja na baadhibya wanafunzi wa chuo hicho  ikiwa ni muendelezo wa ziara  yake ya kukagua maendeleo ya mafunzo ya mfumo wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma kutika Chuo  Ufundi Arusha ( ATC)  yaliyofanyika katika Chuoni hicho.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa  na Mkuu wa Chuo cha Arusha( ATC) Dkt.Musa Chacha wakiangalia baadhi ya mashine za kufundishia wanafunzi kwa vitendo katika chuo hicho kilichopo Jijini Arusha.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Serikali ya wananfunzi wa   Chuo cha Ufundi Arusha ( ATC) mara baada ya kuwasili Chuoni hapo  ikiwa ni muendelezo wa ziara  yake ya kukagua maendeleo ya mafunzo ya mfumo wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma kutika Chuo  Ufundi Arusha ( ATC)  yaliyofanyika katika Chuoni hicho 
Na Lusungu Helela- Arusha 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Ridhiwani Kikwete amesema matumizi ya mfumo wa PIPIMS, PEPMIS na HR Assessment  katika Utumishi wa Umma nchini  itaimarisha Utumishi wa Umma kwa  kuwabana Watumishi wanaopenda kukaa ofisini pasipo kufanya kazi.
Mhe.Kikwete ametoa kauli hiyo leo Jijini Arusha wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na Watumishi wa  Ofisi ya  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha ( AICC) na Chuo cha Ufundi Arusha ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Kupima Utendaji Kazi wa Watumishi wa Umma na Taasisi (PEPMIS na PIPMIS) na Mfumo Maalum wa Tathmini ya hali ya Rasilimaliwatu Serikalini (HR Assessment).
Amesema Serikali imedhamiria kuimarisha Utumishi wa Umma kwa kuhimiza uwajibikaji  ili kuhakikisha kama Taifa linakuwa na utumishi wa umma unaopimika kwa  kumpima Mtumishi mmoja mmoja pamoja  na Taasisi kwa ujumla.
Ameongeza kuwa mfumo wa PEPMIS umekuja kuwa mbadala wa OPRAS ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anayelenga kuimarisha mifumo ya uwajibikaji inayowezesha viongozi na watumishi wa umma kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wakati na mahali popote.
Katika hatua nyingine Mhe. Kikwete amewataka Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala kuacha kukaa ofisini badala yake waende maeneo ya kazi ili kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi walio chini yao.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.John Mongela amesema zama hizi hazihitaji watu wenye misuli kutokana na kukua na teknolojia. Hivyo, teknolojia imerahisisha utendaji kazi na sisi tuko tayari kuisimamia utekelezaji wake.
Amesema ujio wa mafunzo hayo  yamekuja wakati muafaka ambapo  Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wataanza kubadilika na  kuachana na utaratibu wa kizamani wa utendaji kazi wao.
Hata hivyo ametumia fursa hiyo kuiomba Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora kuwanoa upya  Maafisa Utumishi na Maafisa Utawala  wa mikoa na Halmashauri kwani utendaji wao wa kazi sio wa kuridhisha ikizingatiwa wao ndo wenye jukumu la kuwasimamia watumishi wengine.

About the author

mzalendo