Featured Michezo

SARE YAFUFUA MATUMAINI YANGA SC LIGI YA MABINGWA

Written by mzalendoeditor

SARE ya Yanga SC imefufua Matumaini ya kutinga hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1_1 dhidi ya Medeama SC mchezo  Kundi D uliochezwa uwanja wa  Baba Yara Jijini Kumasi nchini Ghana.

Wenyeji walianza kupata bao kupitia kwa Mshambuliaji Jonathan Sowah  kwa penalti dakika ya 27 na katika dakika ya 36 Yanga walipata bao lililofungwa na  kiungo , Pacome Zouazoua.
Mchezo mwingine wa Kundi D Al Ahly imelazimishwa sare ya bila mabao na CR Belouizdad ya Algeria  Uwanja wa Borg El Arab Jijini Alexandria, Misri.
Al Ahly inaendelea kuongoza Kundi D kwa pointi zake tano, ikifuatiwa na CR Belouizdad yenye pointi nne sawa na Medeama, wakati Yanga yenye pointi mbili .

Mechi zijazo, Yanga watawakaribisha Medeama Jijini Dar es Salaam Jumatano ya Desemba 20, wakati Al Ahly watakuwa wageni wa CR Belouizdad Jijini Algiers Jumanne ya Desemba 19.

About the author

mzalendoeditor