Featured Michezo

YANGA SC YABANWA MBAVU KWA MKAPA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Written by mzalendoeditor
UNAWEZA kusema hali sio shwari kwa Yanga SC Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kulazimishwa sare  ya kufungana bao 1-1 na mabingwa watetezi, Al Ahly katika mchezo wa Kundi D uliochezwa  Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza timu zote mbili zilienda mapumziko bila kufungana na kipindi cha pili kilianza kwa kila mmoja kufanya mabadiliko.
Al Ahly walipata bao dakika ya 86 likifungwa na Percy Muzi Tau huku watu wakiamini Yanga hawezi kurudisha bao kutokana na dakika kuwa ukingoni alikuwa kiungo  Fundi kutoka Ivory Coast, Pacôme Zouzoua aliisawazisha Yanga dakika ya 90 +1.
Kwa Matokeo hayo Al Ahly imefikisha pointi nne na kuendelea kuongoza Kundi D kwa pointi moja zaidi ya wote, CR Belouizdad ya Algeria na Medeama ya Ghana, wakati Yanga yenye pointi moja inashika mkia baada ya mechi mbili.
Mechi inafuata Yanga SC itasafiri hadi nchini Ghana kucheza na Medeam  Ijumaa ya Desemba 8, wakati Al Ahly watawakaribisha CR Belouizdad Jijini Cairo.

About the author

mzalendoeditor