Featured Michezo

SIMBA SC YASHINDWA KUTAMBA UGENINI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Written by mzalendo
TIMU ya Simba SC wameshindwa kutamba ugenini katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kulazimishwa sare bila kufungana dhidi ya wenyeji,  Jwaneng Galaxy  mchezo wa Kundi B uliopigwa  Uwanja wa Francistown Jijini Francistown nchini Botswana.
Licha ya kutawala mchezo Simba SC  walishindwa kutumia nafasi walizozipata kutoka kwa wenyeji hao huku wakiwa na Kocha wao Mpya  Mualgeria Abdelhak Benchikha.
Kwa matokeo hayo Simba wamefikisha pointi mbili baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na ASEC Mimosas ya Ivory Coast huku  Jwaneg Galaxy wanafikisha pointi nne baada ya kuanza na ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Wydad Athletic Jijini Marrakech wiki iliyopita.
Simba SC itashuka uwanjani Desemba 9 kucheza na wenyeji Wydad Casablanca nchini Morocco,huku Jwaneng watakuwa wenyeji dhidi ya ASEC Mimosas  hapo hapo Francistown. 

About the author

mzalendo