Featured Kitaifa

WADAU WA MAENDELEO KUENDELEA KUCHANGIA SEKTA ELIMU

Written by mzalendoeditor

Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiongozwa Waziri Prof. Adolf Mkenda imekutana na kuwa na kikao cha pamoja Wadau wa Maendeleo wanaochangia katika Sekta ya Elimu nchini kutoka Balozi na Taasisi mbalimbali za Kimataifa.

Katika kikao hicho wadau wamepongeza juhudi za Serikali katika kuongeza uwekezaji katika elimu na kwa kusimamia vema utekelezaji wa Mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo na Mabadiliko ya Mitaala.

Wadau hao kwa pamoja wameahidi kuendelea kuchangia maendeleo ya elimu ili kujenga nguvu kazi yenye ujuzi kwa maendeleo kupitia utekelezaji wa Sera mpya ya Elimu na Mafunzo.

About the author

mzalendoeditor