Featured Kitaifa

SERIKALI YAAGIZA ELIMU YA FEDHA IWE ENDELEVU

Written by mzalendo
Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini, Felician Mtahengerwa, akizungumza wakati akifunga Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”,yanayofanyika katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja, akitoa maelezo ya awali kuhusu Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayofanyika katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini, Mhe. Felician Mtahengerwa, akimkabidhi Mshindi wa Kwanza wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari kuhusu Umuhimu wa Kuweka Akiba, Usimamizi wa Fedha Binafsi Mikopo, Uwekezaji kwa Maisha Endelevu ya mtu binafsi na jamii, Mwanafunzi Samwel Elisante, wakati wa kufunga Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yanayofanyika katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Wapili kushoto ni Kamishna wa Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja na kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Idara hiyo, Bi. Janeth Hiza.
Meza Kuu ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini, Mhe. Felician Mtahengerwa (aliekaa katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki waliopata tuzo za kufanya vizuri kwenye Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayofanyika katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Meza Kuu ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini, Mhe. Felician Mtahengerwa (aliekaa katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi walioshinda Shindano la Kuandika Insha kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari katika Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayofanyika katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini, Mhe. Felician Mtahengerwa, akimkabidhi Mshindi wa Kwanza wa shindano la uandishi wa insha kwa wanafunzi wa Shule za Msingi, kuhusu Umuhimu wa Kuweka Akiba na Usimamizi wa Fedha, Mwanafunzi Leila Weston Loida wakati wa Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayofanyika katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Katikati ni Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja.
 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha).
Na. Farida Ramadhani na Joseph Mahumi, WF, Arusha
 
Wizara ya Fedha na wadau mbalimbali wa Sekta ya Fedha wameagizwa kuhakikisha Programu ya Elimu ya Fedha kwa Umma inakuwa endelevu ili kuongeza wigo wa uelewa na utumiaji wa huduma za fedha.
 
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini, Mhe. Felician Mtahengerwa, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongella , wakati wa kufunga Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayofanyika katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
 
Mhe. Mtahengerwa alisema kuwa, elimu ya fedha kwa umma isisubiri Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa kwa kuwa wananchi wengi bado wanahitaji elimu ya kutumia huduma rasmi za fedha.
 
Vilevile, ameagiza waratibu na wasimamizi wa sekta ya fedha, kufanya tathmini ya matokeo ya Maadhimisho hayo na elimu ya fedha iliyotolewa kwa umma ili kubaini mafanikio na changamoto kwa ajili ya kuongeza ufanisi.
 
“Ni muhimu sana kufanya tathmini ya matokeo ya maadhimisho haya katika maeneo yaliyowekewa malengo kwa mujibu wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha ili kujua iwapo malengo hayo yamefikiwa”, alisisitiza Mhe. Mtahengerwa.
 
Alisema maeneo ya kuangalia zaidi ni pamoja na kufahamu ongezeko la uelewa wa wananchi na ushiriki wao katika matumizi ya Huduma za Fedha na namna ambavyo elimu hiyo imewasaidia katika kujiendeleza kiuchumi.
 
Aidha, amewasihi wananchi kutumia vyema elimu waliyoipata ili kuitumia katika kuboresha maisha kupitia huduma za fedha. 
 
Akizungumzia Maadhimisho hayo, Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja, alisema maadhimisho hayo ni sehemu utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa Mwaka 2020/21 – 2029/30 ambapo elimu kwa umma ni moja ya maeneo ya kipaumbele katika utekelezaji wa Mpango huo.
 
Dkt. Mwamwaja alisema katika maadhimisho hayo elimu inayotolewa ni pamoja na umuhimu wa kutunza fedha binafsi, kukopa kwa malengo, uwekezaji, umuhimu wa bima pamoja na sheria na sera mbalimbali za fedha zinazomlinda mtumiaji wa huduma za fedha.

About the author

mzalendo