Featured Kitaifa

ASILIMIA 11 YA AKINA MAMA NCHINI HUJIFUNGUA KABLA YA WAKATI KILA MWAKA

Written by mzalendo

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Dkt. Alphonce Chandika,akifafanua jambo kwa  waandishi wa habari na akina Mama waliohudhuria maadhimisho siku ya Kimataifa ya Mtoto Njiti ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 17 ya kila mwaka Duniani kote.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Dkt. Alphonce Chandika,akizungumza na waandishi wa habari na akina Mama  leo Novemba 17,2023 jijini Dodoma waliohudhuria maadhimisho siku ya Kimataifa ya Mtoto Njiti ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 17 ya kila mwaka Duniani kote.

   

Sehemu ya Waandishi wa habari na Wakina Mama wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Dkt. Alphonce Chandika,wakati wa  maadhimisho siku ya Kimataifa ya Mtoto Njiti ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 17 ya kila mwaka Duniani kote.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya watoto Benjamin Mkapa (BMH),Dkt Julieth Kabengula,akielezea sababu za wanawake kujifungua wataoto kabla ya wakati wa  maadhimisho siku ya Kimataifa ya Mtoto Njiti ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 17 ya kila mwaka Duniani kote.

Wakinamama ambao wamejifungia Watoto kabla ya siku kutimia (Njiti),wakitoa shukrani kwa   Madaktari kutoka BMH pamoja na Serikali kuendelea kuboresha huduma za afya katika hospitali.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Dkt. Alphonce Chandika,akiwa katika Picha na Akina Mama wakati wa maadhimisho siku ya Kimataifa ya Mtoto Njiti ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 17 ya kila mwaka Duniani kote

Na.Alex Sonna-DODOMA

KILA ifikapo tarehe 17 ya kila mwaka Duniani kote huadhimisha siku ya Kimataifa ya Mtoto Njiti ambapo imeelezwa asilimia  11 akina Mama milioni mbili hapa nchini hujifungua watoto kabla ya wakati kwa mwaka.

Hayo yameelezwa leo Novemba 17,2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Dkt. Alphonce Chandika wakati wa maadhimisho siku hiyo yaliyobeba kauli mbiu isemayo Vitendo Vidogo,Matokeo Makubwa.

Amesema sababu kubwa ni kutokana na lishe duni wanayopata wajawazito pamoja na kuwepo kwa ugonjwa wa Kisukari,Pressure na maradhi mengine.

”Kila mwaka takribani kinamama milioni mbili nchini hujifungua na kati yao laki mbili na ishirini asilimia 11% ya kinamama hao hujifungua kabla ya wakati (premature delivery).”amesema Dkt. Chandika

Amesema kuwa  zaidi 95% ya watoto hao waliendelea vizuri na kuruhusiwa kutoka hospitali kurudi nyumbani wakiwa na afya njema kama tunavyoona baadhi ya wazazi walioshiriki nasi.

“Niwataarifu kuwa  kati ya watoto 103 watoto walioruhusiwa katika hospital ya Benjamini mkapa ni 98 watoto hawa walizaliwa na umri wa wiki 26 na 27 kitaalamu mimba inayozaliwa wiki 28 inaangaliwa kama abortion, lakini sasa tunaona wanapona na kukua kama Watoto wengine,”.

Amesema kuwa Hospitali ya Benjamin Mkapa imeendelea kutoa huduma kwa watoto wachanga wakiwemo watoto waliozaliwa kabla ya wakati, idadi hii imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka ambapo mwaka 2021 tulihudumia watoto 25 waliozaliwa kabla ya wakati na 2023 watoto 108.

Katika hatua nyingine Dkt  Chandika amesema  wagonjwa ambao wamepata matibabu ya Moyo kwa njia ya kufungua kifua na kutokufungua wameruhusiwa na wanaendelea vizuri.

”BMH  inaendelea kutoa matibabu ya Moyo kwa wagonjwa huku akiwasisitiza jamii iendelee kujitokeza kupata matibabu ya ugonjwa wa Moyo katika hospital hiyo.”amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya watoto Benjamin Mkapa (BMH),Dkt Julieth Kabengula ametoa ushauri kwa jamii hususani wanawake kuandaa mwili kupokea mabadiliko ya ujauzito ili kuepuka kuzaa kabla ya wakati kutokana na changamoto mbalimbali.

“Tunaomba watu wajenge utaratibu wa kuandaa mwili kabla ya kupokea jambo ambalo litawasaidia kujua maradhi waliokuwa kabla ya kushika mimba,”amesema  Dkt Kabengula.

Nao wakinamama ambao wamejifungia Watoto kabla ya siku kutimia (Njiti),wamewashukuru   Madaktari kutoka BMH Hospital huku akiitaka jamii pale wanapoona wana matatizo kipindi cha ujauzito waende kwa wataalam kupata matibabu ili kujifungua salama.

Hospitali ya Benjamini Mpaka tangu kuanzishwa kwake imeendelea kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa utumbo nje ambapo mpaka sasa watoto watano kati ya 15 waliowahi kulazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu wameruhusiwa na kurudi nyumbani.

Siku ya watoto waliozaliwa kabla ya wakati ilianzishwa kwa nia ya kuelimisha kuhusu kujifungua watoto ambao bado hawajakomaa.

About the author

mzalendo