Uncategorized

WATAALAMU WA TEHAMA NCHINI WATAKIWA KUBUNI MIFUMO BORA YA AFYA

Written by mzalendo

Kuelekea Bima ya Afya kwa Wote, Wataalamu wa Tehama nchini wametakiwa kuhakikisha wanakuwa wabunifu katika mifumo inayotumika katika zahanati inasomana na Hospitali za Taifa ili kumuondolea mwananchi usumbufu wa kupata huduma pale wanapopewa rufaa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel leo Novemba 16, 2023, wakati alipomwakilisha Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu katika Ufunguzi wa Maonyesho ya tatu ya wiki ya Kidigitali ya Afya na Ubunifu yanayofanyika katika chuo cha Afya na Sayansi Muhimbili kampasi ya Mloganzila.

Amesema mifumo katika sehemu za kutolea huduma za afya itasaidia kuondoa usumbufu kwa wanachi wa kutorudia vipimo pale watakapo kuwa wamepewa Rufaa ya kwenda kupata Huduma katika ngazi yoyote nchini.

Vile vile ameongeza kuwa Mifumo katika hospitali zote nchini inatakiwa kusomana na Mfuko wa Bima ya Afya nchini ili kuboresha Huduma na kuondoa misongamano katika hospitali.

“Kwa mtaalam yeyote wa afya atakaye rudia kufanya vipimo bila sababu za kitabibu atachukuliwa hatua kwa kutofata utaratibu wa kutumia mifumo iliyosimikwa kwani Serikali ya Rais Samia imefanya uwekezaji mkubwa sana katika Sekta ya afya nchini”. Amesisitiza Dkt. Mollel.

Lakini pia Dkt. Mollel ametaka mfumo wa Hospitrali zote kuwa kusomana na Bohari ya Dawa ili kusaidia upatikanaji wa dawa na kujua dawa gani inatumika sana katika maeneo yapi na wapi hawatumii dawa hioz na zielekjezwe katika maeneo yenye uhitaji zaidio.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI, Dkt. Ndungulile ametoa wito kwa serikali kuhakikisha wizara ya afya na TAMISEMI wanashirikiana kwa karibu ili mifumo kusomana kwa ufasaha na kuleta tija kwa wananchi.

About the author

mzalendo