Uncategorized

MPANGO WA UTEKELEZAJI WA HUDUMA YA CHAKULA NA LISHE SHULENI WAZINDULIWA DODOMA

Written by mzalendo

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Miundombinu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Reagatus Mativila,akiwa na Viongozi wakionyesha Miongozo mara baada ya kuzindua mpango wa utekelezaji wa mwongozo wa kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa Elimumsingi hafla iliyofanyika leo Novemba 16,2023 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Na.Alex Sonna-DODOMA

 
SERIKALI imezindua Mpango wa Utekelezaji wa Mwongozo wa Kitaifa wa utoaji wa Huduma ya Chakula na Lishe kwa wanafunzi wa elimu ya msingi huku ikilipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwa kufanya sensa ya utoaji wa huduma hiyo Mashuleni.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Miundombinu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Reagatus Mativila,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango huo uliofanyika leo Novemba 16,2023 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.
 Mhandisi Mativila, amesema kuwa  Serikali inatambua mchango wa wataalam kutoka wizara,taasisi na wadau mbalimbali walioshiriki kuandaa mpango huo..
 
“Kwa kipekee Ofisi ya Rais TAMISEMI, inatoa shukrani za dhati kwa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwa kufanya sensa ya utoaji wa huduma ya chakula na lishe katika shule za msingi nchini”amesema Mhandisi Mativila
 
Aidha Mhandisi Mativila amesema kuwa  matokeo yaliyopatikana na kuwasailishwa serikalini ni chachu katika utekelezaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni.
 
“Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa kuchapisha nakala 33,000 za vitabu ambavyo vinazinduliwa leo kwa ajili ya kusambazwa katika shule zote za msingi na sekondari nchini”amesema 
 
Amesema kuwa  vitabu hivyo vitawezesha kuweka malengo ya Mwongozo wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe katika vitendo kwa ajili ya utekelezaji.
 
Hata hivyo Mhandisi Mativila amesema  kwa sasa utoaji wa chakula na lishe shuleni umegawanyika katika makundi mawili.
 
 ”Kundi la kwanza ni la wanafunzi wa bweni ambao wanahudumiwa na serikali na jingine ni wanafunzi wa kutwa ambao wanahudumiwa na wadau mbalimbali wakiwemo wazazi, jamii, taasisi za dini na Makampuni.”amesema 
 
Kwa upande wake Awali Mwakilishi Mkazi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)Bi.Sarah Gordon Gibson,amesema programu ya kutoa chakula shuleni inalenga kuhakikisha ajenda ya maendeleo ya mtaji wa binadamu hasa ongezeko la uandikishaji wanafunzi kwa asilimia 9 na mahudhurio asilimia 10,kukuza usawa wa jinsia na kuongeza wanafunzi wa kike shuleni.
”Programu hii inasaidia kilimo,masoko na kukuza uchumi wa ndani kupitia uzalishaji ajira 1700 kwa kila watoto 100,000 wanaolishwa shuleni hivyo ni lazima jamii iwekeze kwa watoto  ili kuwepo utoaji nzuri wa chakula siku zijazo”amesema Bi.Sarah
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,amesema kuwa utekelezaji wa Mwongozo huo unategemea ushiriki wa makundi yote ikiwemo wazazi, serikali pamoja na wadau wengine wa maendeleo.
 
“Wazazi wanapopanga bajeti zao za chakula nyumbani hawanabudi kutambua kuwa ipo haja wao pia kutenga bajeti kwa ajili ya watoto wao kupata chakula wanapokuwa shule ili kuwawezesha kushiriki vipindi na kuondokana na tatizo la utoro”amesema Prof.Mdoe
 
Prof.Mdoe amesema kuwa  utoaji wa chakula shuleni ni jambo muhimu katika kuwasaidia watoto kushiriki masomo kwa mujibu wa ratiba ili kuongeza ufaulu.
 
“Chakula ni kitu muhimu sana kwa kila mtu hivyo uwepo wa Mwongozo huu wa utoaji wa chakula na lishe shuleni utakuwa na msaada mkubwa kwa watoto wetu katika ushiriki wao wa masomo na kuwaongezea usikuvu tofauti na ilivyo sasa”amesema 
 
Aidha amesema kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itaendelea kushirikiana kwa pamoja kuhamasisha wazazi na wadau wengine ili kuchangia kwenye shule zote nchini na watoto wote kupata chakula kwa asilimia 100.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Miundombinu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Reagatus Mativila,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa utekelezaji wa mwongozo wa kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa Elimumsingi iliyofanyika leo Novemba 16,2023 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Mkurugenzi wa Elimu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ….akielezea lengo la  uzinduzi wa mpango wa utekelezaji wa mwongozo wa kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa Elimumsingi uliofanyika leo Novemba 16,2023 jijini Dodoma.

Mwakilishi Mkazi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)Bi.Sarah Gordon Gibson ,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa utekelezaji wa mwongozo wa kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa Elimumsingi iliyofanyika leo Novemba 16,2023 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa utekelezaji wa mwongozo wa kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa Elimumsingi iliyofanyika leo Novemba 16,2023 jijini Dodoma.

Baadhi ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Miundombinu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Reagatus Mativila (hayupo pichani),akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa utekelezaji wa mwongozo wa kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa Elimumsingi iliyofanyika leo Novemba 16,2023 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Medeli na Shule ya Sekondari ya Kiwandani wakifatilia  hafla ya uzinduzi wa mpango wa utekelezaji wa mwongozo wa kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa Elimumsingi iliyofanyika leo Novemba 16,2023 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Miundombinu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Reagatus Mativila,akikata utepe kuashiria  uzinduzi wa mpango wa utekelezaji wa mwongozo wa kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa Elimumsingi hafla iliyofanyika leo Novemba 16,2023 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Miundombinu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Reagatus Mativila,akiwa na Viongozi wakionyesha Miongozo mara baada ya kuzindua mpango wa utekelezaji wa mwongozo wa kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa Elimumsingi hafla iliyofanyika leo Novemba 16,2023 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Miundombinu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Reagatus Mativila,akikabidhi Miongozo kwa wadau mbalimbali mara baada ya kuzindua  mpango wa utekelezaji wa mwongozo wa kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa Elimumsingi hafla iliyofanyika leo Novemba 16,2023 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Miundombinu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Reagatus Mativila,akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Msingi Medeli na Wanafunzi wa Sekondari ya Viwandani mara baada ya kuzindua  Mpango wa utekelezaji wa mwongozo wa kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa Elimumsingi hafla iliyofanyika leo Novemba 16,2023 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Miundombinu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Reagatus Mativila,akiwa katika picha ya pamoja na Wadau mbalimbali  mara baada ya kuzindua  Mpango wa utekelezaji wa mwongozo wa kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa Elimumsingi hafla iliyofanyika leo Novemba 16,2023 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Miundombinu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Reagatus Mativila,akiagana na Mwakilishi Mkazi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)Bi.Sarah Gordon Gibson  mara baada ya kuzindua  Mpango wa utekelezaji wa mwongozo wa kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa Elimumsingi hafla iliyofanyika leo Novemba 16,2023 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.

About the author

mzalendo