Uncategorized

RAIS DK.MWINYI AFUNGUA MKUTANO WA UFADHILI WA USAWA WA KIJINSIA NCHI 22 AFRIKA

Written by mzalendo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Tanzania imepitisha na kutekeleza mageuzi kadhaa ya kisera yakiwemo marekebisho ya hivi karibuni ya sera ya maendeleo ya jinsia ya Tanzania ambayo yameweka mfumo wa kuimarisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake katika masuala ya elimu, afya, ajira na upatikanaji wa ardhi.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akifungua mkutano wa Mawaziri wa Afrika wanaohusika na fedha pamoja na jinsia kutoka nchi 22 wanachama kwa kushirikiana na jukwaa la usawa wa kijinsia(UN WOMEN) na shirika la fedha la kimataifa (IMF Afritac East) ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana, Dar es Salaam tarehe 15 Novemba 2023.

Mkutano huo utajadili kuhusu ufadhili wa usawa wa kijinsia.

Vilevile Nchi zinazoshiriki mkutano huo ni pamoja na wenyeji Tanzania, Burundi, Burkina Faso, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Eritrea, Ethiopia, Guinea, Ivory Coast, Nigeria, Senegal, Kenya, Liberia, Madagascar, Malawi, Msumbiji, Somalia, Afrika Kusini, Rwanda, Sudan ya Kusini, Zambia, Zimbabwe na Uganda .

Mashirika mbalimbali ya kimataifa wanashiriki mkutano huo unaoendelea hadi tarehe 17 Novemba.

Naye Waziri wa fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mwigulu Nchemba amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ni nguzo ya mafanikio kwa Wanawake nchini kutokana na uongozi wake, pia Serikali imeendelea kupigania usawa wa kijinsia na kuwawezesha Wanawake nchini.

ūüďćHoteli ya Johari Rotana, Dar es Salaam.

About the author

mzalendo