Wazee wa Butiama Mkoani Mara wamemkabidhi Kifimbo Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Paul Makonda kama ishara ya Uongozi bora na Ukumbusho wa kumtaka aendelee hivyohivyo kumuenzi Hayati Mwl. Julius K. Nyerere.
Tukio hilo limafanyika wakati Mwenezi Makonda akitokea Bunda mara baada ya kumaliza Mkutano wa Hadhara ambapo alipofika maeneo ya Nyamuswa Wazee hao pamoja na Wananchi wangine walisimamisha msafara wake, leo tarehe 13 Novemba, 2023