Featured Kitaifa

MAKONDA:WANAOMKANA HAYATI MAGUFULI RAIS SAMIA ANAWATAZAMA ANAJUA IPO SIKU MTAMKANA NA YEYE

Written by mzalendo

“Mimi ni muumini wa kutambua chanzo cha baraka, kama hutambui chanzo chako cha baraka zako zimeanzia wapi basi atakayekupa baraka kwasasa bado hutomshukuru, ni vema kushukuru na kutambua baraka ulizopewa”

“Wanasiasa wenzangu niwaambie tu ukweli msisahau watu waliowashika mikono, wapo watu wanamsema vibaya Hayati Magufuli na kumsahau mema aliyowatendea na watu kama hao maana yake siku moja watakuja kusahau mema wanayotendewa na Rais Samia”

“Rais Samia ni Mama mwenye hekima na busara kubwa mno, anatumia sana akili na anawaangalia tu mnaomkana Hayati Magufuli anajua ipo siku mtamkana na yeye kwahiyo kuweni na upendo wa kweli, Chama Cha Mapinduzi kimetulea na kutufunza naamini hatujafunzwa kuwa wanafiki.”

Cde. Paul Makonda
Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa.

Akizungumza njiani na Wananchi wa Sengerema Jijini Mwanza kwenye ziara yake leo tarehe 12 Novemba, 2023.

#CCMKazini
#VitendoVinaSauti
#KaziIendelee

About the author

mzalendo