Featured Kitaifa

CCM YABAINI RUSHWA NA USIMAMIZI NDIO CHANZO CHA UCHEREWESHWAJI WA BAADHI YA MIRADI NCHINI

Written by mzalendo

 

“Tumuunge mkono Rais wetu anayo nia na njia njema na ameendelea kutoa pesa nyingi katika kila Mkoa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Nchi nzima”

“Lakini Chama Cha Mapinduzi kupitia ziara zinazofanywa, tumebaini Rushwa ni chanzo cha kwanza kinachopelekea uchereweshwaji katika kutekeleza baadhi ya Miradi lakini na hata mingine kukamilika chini ya kiwango stahiki”

“Pia tumebaini chuki baina ya Viongozi walioaminiwa katika Serikali nayo ni sababu, unakuta kiongozi fulani hana maelewano na mwingine mwishowe kuwekeana majungu, ugomvi na kupelekea kazi kutofanyika kwa wakati ama inavyostahili”

“Sasa Chama Cha Mapinduzi kitachukua hatua katika hili na ndio maana jana nikiwa Mkoani Geita nilielekeza Kamati za Siasa Wilaya na Mikoa kutokaa kimya kwa watumishi wote wabaokuwa chanzo cha kukwanisha maendeleo, lazima wachukuliwe hatua”

Cde. Paul Makonda
Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa.

AKizunguma njiani na Wananchi wa Sengerema Jijini Mwanza kwenye ziara yake leo tarehe 12 Novemba, 2023.

#CCMKazini
#VitendoVinaSauti
#KaziIendelee

About the author

mzalendo