Na Mwandishi wetu.
Taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance imemkabidhi Bi ummy Kuruthumu mkazi wa zanzibar zawadi yake ya simu janja baada ya kuibuka mshindi katika droo ya tatu ya kampeni ya pakua App ya Y9 Microfinance na kupata huduma tatu ambazo ni mkopo wa fedha taslimu
Ummy alikabidhiwa zawadi hiyo na Meneja Masoko wa Taasisi ya Y9 Microfinance, Sophia Mang’enya ambaye pia alieleza kuwa hiyo ni fursa kubwa kwa watanzania, kwani Taasisi ya Y9 imekuja kuwa mkombozi kwa Watanzania hata wale wenye kipato cha chini.
“Nawapongeza washindi wote kwa kujiunga na huduma zetu na kuweza kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo simu, pikipiki ,lakini hata hivyo napenda kuongeza kuwa droo ya mwisho ambayo itafanyika katikati ya mwezi Desemba, kutakuwa na zawadi kubwa zaidi ya gari aina ya Toyota IST”,alisema Mang’enya.
Alisema kuwa washindi hao wameshinda zawadi hizo baada ya kupakuwa ‘App’ yeo na kukopa kupitia ‘App’ na kurejesha mikopo yao ndani ya muda uliowekwa kwa mujibu wa taratibu zao.
Amefafanua kuwa zawadi bado zipo nyingi na amewaomba Watanzania kuendelea kutumia huduma zao. “ Tumekuwa na muendelezo wa kuchezesha droo kila wiki na kutoa zawadi kila wiki kwa washindi wetu, leo pia tumechezesha droo na kupata washindi wawili kutoka mikoa ya Rukwa, Bwa Boniface Senga ambae amejishindia simu janja na mshindi wa pili ni Bwa Iddi Kiruvia kutoka Njombe ambae amejishindia pikipiki.
Kwa upande wake, Afisa Msimamizi wa michezo ya bodi ya kubahatisha nchini, Salim Mkufi aliwapongeza washindi hao kwa kuiamini Taasisi ya Y9 na kuwaomba Watanzania kutumia fursa hiyo ili kufikia malengo yao.
Mkufi pia ameipongeza Taasisi ya Y9 kwa namna ilivyoweza kuwafikia vijana wengi wa kitanzania na kuwapa mikopo kwa masharti rafiki na kuwataka waendelee kuongeza wigo kutanua huduma zao ila kila mtanzania anufaike na mikopo hiyo.
Meneja Masoko wa Taasisi ya Y9 Microfinance, Sophia Mang’enya akikabidhi zawadi ya simu janja kwa Bi Ummy Kuruthumu mkazi wa Zanzibar ambae ni mshindi wa droo ya tatu ya pakua App ya Y9 USHINDE kwaajili yakujipatia huduma mbalimbali za kifedha kama vile kununua Umeme, muda wa maongezi. Kushoto ni Afisa Msimamizi wa michezo ya bodi ya kubahatisha nchini, Salim Mkufi akishuhudia tukio hilo.