Featured Kitaifa

WAZIRI HAROUN ALI SULEIMAN MGENI RASMI MKUTANO WA ACFET

Written by mzalendo

 

 Rais wa Taasisi ya Wataalamu dhidi ya Rushwa na Ufisadi Tanzania (ACFET) Bw.Ali Mabrouk Juma,akizungumza leo  Novemba 2,2023 jijini Dodoma na waandishi wa habari (hawapo pichani)  wakati akitoa taarifa  kuhusu Mkutano wa Taasisi hiyo unaotarajiwa  kuanzia Novemba 6 hadi 10,2023  jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Taasisi ya Wataalamu dhidi ya Rushwa na Ufisadi Tanzania (ACFET) Bw.Stephen Obado Agwanda,akifafanua zaidi kuhusu  kuhusu Mkutano wa Taasisi hiyo unaotarajiwa  kuanzia Novemba 6 hadi 10,2023  jijini Arusha.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI  wa Nchi, Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Taasisi ya wataalamu dhidi ya Rushwa na Ufisadi Tanzania (ACFET) utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Novemba 6 hadi 10,2023 ambapo utahusisha watumishi kutoka taasisi mbalimbali kutoka nchini na nje ya nchi.

Hayo yameelezwa leo Novemba 2,2023 jijini Dodoma na Rais wa Taasisi ya Wataalamu dhidi ya Rushwa na Ufisadi Tanzania (ACFET) Bw.Ali Mabrouk Juma wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mkutano huo.

Bw.Juma amesema kuwa  Mkutano huo utawakutanisha Wadau mbalimbali wanaopinga vitendo vya Rushwa kutoka Mataifa mbalimbali na Mada mbalimbali zitawasilishwa.

“Mada kuu katika mkutano huu itakuwa ni mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi katika kujenga uchumi lakini pia katika kusimamia miradi ya maendeleo hiyo itakuwa mada kuu katika mkutano huu,” amesema Bw.Juma

Hata hivyo ameongeza kuwa kazi kubwa inayofanywa na taasisi hiyo ni kutoa elimu kwa wananchi pamoja na taasisi mbalimbali na kupeleka wataalamu wengine nje ya nchi kwenda kupata ujuzi zaidi katika kukabiliana na changamoto ya rushwa na ufisadi.

“Baada ya kuwapeleka wataalamu hawa kwenda kupata ujuzi Marekani, hivi sasa tumeandaa Mazingira ya wao kupata elimu hapa hapa nchini kutokana na gharama za kuwapeleka nje ya nchi kuwa kubwa,”amesema.

Awali Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo Bw.Stephen Obado Agwanda  amesema kuwa taasisi hiyo pia inaandaa wataalamu na wanapokuwa wameivaa wanazishawishi taasisi mbalimbali kuwa na wataalamu wanawezesha mapambano ya rushwa na ufisadi yanakomeshwa katika maeneo yao.

“Kwahiyo wanapokuwa wameajiriwa katika maeneo hayo kazi yao ni kuweka mifumo dhabiti ya kuhakikisha hatufikii mwisho mpaka mmepata tatizo ndiyo muanze kwenda kwenye vyombo vya uchunguzi lakini pia taasisi yetu ina mashirikiana makubwa na vyombo vya uchunguzi kama TAKUKURU,”amesema Bw.Stephen Obado Agwanda

About the author

mzalendo