Featured Michezo

SPIKA WA BUNGE ATETA NA MWENEZI WA CCM NDUGU PAUL MAKONDA

Written by mzalendo

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Paul Makonda Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 2 Novemba, 2023.

Pamoja na Mambo mengine, Makonda amempongeza Dkt. Tulia kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa IPU ambapo amesema kuwa CCM itahakikisha inamuunga mkono katika majukumu yake ili azidi kuitangaza Tanzania kimataifa.

About the author

mzalendo