Featured Michezo

KOMREDI LULANDALA ATETA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MPIRA WA WAVU TANZANIA

Written by mzalendo

Na.Mwandishi Wetu_Upanga Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa Komredi Fakii Raphael Lulandala (MNEC), amezungumza na Viongozi wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (Tanzania Volleyball Association – TAVA) katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Upanga Jijini Dar es Salaam Viongozi hao ni Mhandisi, Magoti Mtani, Mwenyekiti na Ndugu Laurance Safari Katibu Mkuu.

Lengo la Mazungumzo hayo ilikua kusikiliza Changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi, kutafuta namna bora ya kuufanya mchezo wa wavu kuwa fursa ya ajira kwa vijana kama ilivyo kwa mpira wa miguu na zaidi kudumisha Ushirikiano kati ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi na (TAVA) ambao ni chanzo cha kukuza Vipaji vya Vijana wengi nchini.

Pamoja naye Katibu Mkuu alikuwa na Manaibu makatibu wakuu wa Jumuiya Komredi Mussa Mwakitinya (MNEC) Naibu Katibu Mkuu Bara na Komredi Mussa Haji Mussa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

#KulindaNaKujengaUjamaa
#SisiNaMamaMleziWaWana
#Kaziiendelee

Imetolewa na
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM-Taifa

About the author

mzalendo