Featured Michezo

WAZIRI NDUMBARO APIGIA “DEBE” FILAMU ZA TANZANIA KIMATAIFA

Written by mzalendo

Na Brown Jonas

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Oktoba 27, 2023 Jijini Dar es Salaam ameungana na Raia wa Uturuki wanaoishi hapa nchini kusherehekea miaka 100 tangu kuanzishwa kwa taifa hilo.

Akizungumza katika hafla hiyo Dkt. Ndumbaro amesema kuwa, Tanzania itendelea kushirikiana na nchi hiyo katika maeneo mbalimbali hususani kuendeleza Sanaa ya Tanzania hasa filamu ili ziweze kufika kiwango cha juu.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Mabalozi Pamoja na viongozi wengine wa kidiplomasia.

About the author

mzalendo