Featured Kitaifa

WAZIRI MAKAMBA APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MWAKILISHI MKAZI WA UNDP

Written by mzalendo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akipokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akipeana mikono na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara baada ya kupokea Hati za Utambulisho za mwakilishi huyo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara baada ya kupokea Hati za Utambulisho za mwakilishi huyo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) baada ya kukabidhi Hati zake za Utambulisho katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) katika picha na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara baada ya kupokea Hati za Utambulisho za mwakilishi huyo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) na ujumbe wake (kulia) katika picha na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara na ujumbe wake (kushoto) baada ya kupokea Hati za Utambulisho za mwakilishi huyo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

………….

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amepokea Hati za Utambulisho za mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kupokea nakala za hati hizo, Mhe. Waziri Makamba amemhakikishia Bw. Komatsubara kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na UNDP ili kusogeza mbele agenda yake ya maendeleo na hivyo kuinua maisha ya watanzania kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Mhe. Waziri amesema Tanzania na UNDP zimekuwa zikishirikiana kutekeleza mipango ya maendeleo kwa kuwa zina lengo la kuboresha maisha ya watu kupitia maeneo ya utawala wa demokrasia, ukuaji uchumi, maendeleo endelevu  mazingira endelevu na uhimilivu wa mabadiliko ya tabia nchi.

Waziri Makamba ameongeza kuwa Tanzania inathmini na kutambua jitihada za UNDP katika kukabiliana na madhara yaliyotokana na janga la UVIKO 19

Kwa upande wake Mwakilishi wa UNDP nchini, Bw. Komatsubara ameahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuendeleza jitihada za UNDP nchini na kuongeza kuwa atakuwa sio tu Balozi mzuri wa Tanzania bali pia atakuwa mtangaza mazuri ya Tanzania kupitia kazi zake.

Bw. Komatsubara ameongeza kuwa ofisi yake ina nia ya kusaidia Tanzania kujenga uwezo kwa watu wake ili kutekeleza kwa ufanisi mipango ya maendeleo na kwamba atahakikisha UNDP inaendelea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha  ajenda ya maendeleo inafanikishwa.

About the author

mzalendo