Featured Kitaifa

SERIKALI YAPONGEZA MAFANIKIO YA MRADI WA HPSS TUIMARISHE AFYA

Written by mzalendoeditor

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk.Festo Dugange,akizungumza wakati  akifunga kikao cha siku mbili cha kuhitimisha mradi wa HPSS Tuimarishe Afya uliokuwa ukitekelezwa kwa kushirikiana na TAMISEMI na Wizara ya Afya kwa ufadhili wa serikali ya Uswisi kilichofanyika jijini Dodoma.

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk.Festo Dugange,akiongoza na Meneja Mradi wa HPSS – Tuimarishe Afya Bw.Ally Kebby wakati akiingia ukumbini kwa ajili ya kufunga kikao cha siku mbili cha kuhitimisha mradi wa HPSS Tuimarishe Afya uliokuwa ukitekelezwa kwa kushirikiana na TAMISEMI na Wizara ya Afya kwa ufadhili wa serikali ya Uswisi.

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk.Festo Dugange,akizungumza wakati  akifunga kikao cha siku mbili cha kuhitimisha mradi wa HPSS Tuimarishe Afya uliokuwa ukitekelezwa kwa kushirikiana na TAMISEMI na Wizara ya Afya kwa ufadhili wa serikali ya Uswisi kilichofanyika jijini Dodoma.

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk.Festo Dugange,akizungumza wakati  akifunga kikao cha siku mbili cha kuhitimisha mradi wa HPSS Tuimarishe Afya uliokuwa ukitekelezwa kwa kushirikiana na TAMISEMI na Wizara ya Afya kwa ufadhili wa serikali ya Uswisi kilichofanyika jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Makatibu Tawala wa Mikoa, Rehema Madenge,akizungumza wakati  wa kikao cha siku mbili cha kuhitimisha mradi wa HPSS Tuimarishe Afya uliokuwa ukitekelezwa kwa kushirikiana na TAMISEMI na Wizara ya Afya kwa ufadhili wa serikali ya Uswisi kilichofanyika jijini Dodoma.

 Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde ,akizungumza wakati wa  kikao cha siku mbili cha kuhitimisha mradi wa HPSS Tuimarishe Afya uliokuwa ukitekelezwa kwa kushirikiana na TAMISEMI na Wizara ya Afya kwa ufadhili wa serikali ya Uswisi kilichofanyika jijini Dodoma.

WASHIRI wakimsikiliza Naibu  Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk.Festo Dugange,(hayupo pichani)  wakati  akifunga kikao cha siku mbili cha kuhitimisha mradi wa HPSS Tuimarishe Afya uliokuwa ukitekelezwa kwa kushirikiana na TAMISEMI na Wizara ya Afya kwa ufadhili wa serikali ya Uswisi kilichofanyika jijini Dodoma.

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk.Festo Dugange,akiwa katika picha mara baada ya kufunga  kikao cha siku mbili cha kuhitimisha mradi wa HPSS Tuimarishe Afya uliokuwa ukitekelezwa kwa kushirikiana na TAMISEMI na Wizara ya Afya kwa ufadhili wa serikali ya Uswisi kilichofanyika jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

SERIKALI imeahidi kuendeleza mafanikio ya mradi wa HPSS Tuimarishe Afya kwa kuweka mikakati ya kutosha katika kuboresha ubora wa huduma za afya nchini.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Naibu  Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk.Festo Dugange, wakati akifunga kikao cha siku mbili cha kuhitimisha mradi wa HPSS Tuimarishe Afya uliokuwa ukitekelezwa kwa kushirikiana na TAMISEMI na Wizara ya Afya kwa ufadhili wa serikali ya Uswisi.

Dkt.Dugange amebainisha maeneo ambayo mradi umefanya kazi ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa (iCHF) mshitiri pamoja na uimarishaji wa utengenezaji wa vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Aidha amesema kuwa  serikali imefanya kazi kubwa ya ujenzi wa zahanati, vituo vya afya, Hospitali za Wilaya, Mikoa na rufani na kwasasa nguvu kubwa inaelekezwa katika kuboresha huduma kwa kuwa bado kuna pengo kwenye eneo hilo.

“Tunatumia fedha nyingi sana kununua vifaa tiba mara kwa mara vinatumika kwa muda mfupi na kushindwa kufanya marekebisho madogo, mradi wa HPSS Tuimarishe Afya umetuwezesha namna ya kuweka mifumo imara ya matengenezo ya mara kwa mara ya vifaa tiba na miundombinu mingine ili kutoa huduma vizuri,”amesema Dkt.Dugange

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Makatibu Tawala wa Mikoa, Rehema Madenge, amesema mradi huo umeleta utaratibu wa mshitiri umesaidia upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za dawa pale ambapo hazipatikani kutoka MSD kwa wakati.

About the author

mzalendoeditor