Featured Kitaifa

MRADI WA ELIMU YA JUU KWA MAGEUZI YA KIUCHUMI CHUO KIKUU MZUMBE WAENDESHA MAFUNZO KWA WAHADHIRI KUHUSU UFUNDISHAJI WA KIBUNIFU

Written by mzalendoeditor

Kaimu  Mratibu wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) Dkt. Hawa Tundui, akimkaribisha Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William  Mwegoha kufungua Mafunzo ya Wahadhiri juu ya kuunganisha ufundishaji wa kibunifu na masuala mtambuka katika mitaala yanayoendelea  katika Hoteli  ya Oasis, Morogoro. Mafunzo hayo yameratibiwa na Mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET- Project) Chuo Kikuu Mzumbe.

Dkt. Perpetua Kalimasi akifundisha kamati zinazotengeneza na kupitia mitaala za Chuo Kikuu Mzumbe kuhusu Rasimu ya mitaala ya Elimu ya msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu ili waweze kuhusisha na mitaala wanayoihuisha katika mafunzo ya wahadhiri juu ya kuunganisha ufundishaji wa kibunifu  na masuala mtambuka katika mitaala yaliyofanyika katika Hotel ya Oasis Morogoro.

Washiriki wa Mafunzo ya Wahadhiri juu ya kuunganisha ufundishaji wa kibunifu na masuala mtambuka katika mitaala wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilika kwa hafla ya ufunguzi. Mafunzo hayo yameratibiwa na Mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET-Project) Chuo Kikuu Mzumbe

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha akifungua Mafunzo yaliyoshirikisha Wahadhiri kutoka Chuo Kikuu Mzumbe  juu ya kuunganisha ufundishaji wa kibunifu na masuala mtambuka katika mitaala, katika mafunzo yanayoendelea  katika Hoteli  ya Oasis, Morogoro. Mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET-Project) Chuo Kikuu Mzumbe ndio umeratibu mafunzo hayo ya siku tatu

Dkt. Joseph Sungau (Mratibu kuhuisha na kuanzisha mitaala upande wa HEET Project) akielezea kuhusu kuhuisha na kuanzisha mitaala katika Mafunzo ya wahadhiri juu ya mbinu bunifu katika ufundishaji na mambo mtambuka katika mitaala yanayoendelea  katika Hoteli  ya Oasis, Morogoro. Mafunzo hayo yameratibiwa na Mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET-Project) Chuo Kikuu Mzumbe na yamefunguliwa na Kaimu Mkuu wa Chuo Prof. William Mwegoha

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha (katikati) akiwa na wawezeshaji wa Mafunzo ya Wahadhiri juu ya kuunganisha ufundishaji wa kibunifu na masuala mtambuka katika mitaala yanayoendelea  katika Hoteli  ya Oasis, Morogoro. Mafunzo hayo ya siku tatu yameratibiwa na Mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET-Project) Chuo Kikuu Mzumbe.

About the author

mzalendoeditor