Featured Kitaifa

MPANJU ATAKA VIONGOZI NGAZI YA KATA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Written by mzalendoeditor

Naibu Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na makundi maalum Wakili Amon Mpanju,akizungumza  wakati akifungua matunzo ya Mpango wa Taifa wa Kuhamasisha na kusimamia maendeleo ngazi ya msingi kwa Wataalam wa ngazi ya Kata Jijini leo Oktoba 5,2023 jijini Dodoma.

Mkurugenzi idara ya maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na makundi maalum Bw.Patrick Golwike,akizungumza  wakati wa   mafunzo ya Mpango wa Taifa wa Kuhamasisha na kusimamia maendeleo ngazi ya msingi kwa Wataalam wa ngazi ya Kata Jijini leo Oktoba 5,2023 jijini Dodoma.

  Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na makundi maalum Wakili Amon Mpanju,(hayupo pichani) wakati wa  mafunzo ya Mpango wa Taifa wa Kuhamasisha na kusimamia maendeleo ngazi ya msingi kwa Wataalam wa ngazi ya Kata Jijini leo Oktoba 5,2023 jijini Dodoma.

Katibu Tawala Mipango,uratibu wa Mkoa wa Dodoma Bw.Charles Mduma,akizungumza wakati wa Mkutano wa matunzo ya Mpango wa Taifa wa Kuhamasisha na kusimamia maendeleo ngazi ya msingi kwa Wataalam wa ngazi ya Kata Jijini leo Oktoba 5,2023 jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Francis Kilawe,akizungumza wakati wa Mkutano wa mafunzo ya Mpango wa Taifa wa Kuhamasisha na kusimamia maendeleo ngazi ya msingi kwa Wataalam wa ngazi ya Kata Jijini leo Oktoba 5,2023 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na makundi maalum Wakili Amon Mpanju,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua  mafunzo ya Mpango wa Taifa wa Kuhamasisha na kusimamia maendeleo ngazi ya msingi kwa Wataalam wa ngazi ya Kata Jijini leo Oktoba 5,2023 jijini Dodoma.

Na James Nestory -DODOMA

Naibu Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na makundi maalum Wakili Amon Mpanju amewataka Viongozi wataalamu ngazi ya kata kuhakikisha wanaweka mpango kazi unaopimika wa utekelezaji maendeleo ngazi ya masingi kwenye maeneo yao ili kuakisi maudhui ya mpango wa kitaifa unaosimamia maendeleo.

Hayo yameelezwa leo October 5,2023Jijini Dodoma  wakati akifungua mafunzo ya Mpango wa Taifa wa Kuhamasisha na kusimamia maendeleo ngazi ya msingi kwa Wataalam wa ngazi ya Kata Jijini wenye lengo la kuhamasisha maendeleo ngazi ya msingi na kuwafanya wananchi kuwa kitovu cha maendeleo kwa kutumia rasilimali zilizoko kwenye maeneo yao.

Ili kufanikiwa kwa Mpango huo amewaagiza watendaji wa Kata na Vijiji kutoka ofisini kwenda kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua kwa wakati na kwamba hali hiyo itasaidia wananchi kuendelea kuiamini Serikali.

“Nawasihi mkawajibike kwa kufanya kazi zenye matokeo kwa kuzingatia umoja na uzalendo kwa kushirikishana ngazi na kata kuheshimiana kwa taaluma mshirikishane ujuzi na maarifa mchape kazi kama timu ndo mtaweza kufikia nia ya watanzania kuwa kitovu cha maendeleo ngazi ya msingi, “amesema na kuongea,

Hivi vyote vifanyike na kila mtu kwenye eneo lake awasilishe taarifa ya kina ya uwajibikaji wake namna anavyowahudumia wananchi ili mfanye tathmini kwa pamoja na kuweka mkakati wa maboresho, ” Amesisitiza

Mbali na hayo Naibu Waziri huyo mwenye dhamana ya maendeleo ya Jamii amesema, “Mkiyaishi hayo tutakuwa na matokeo tarajiwa wananchi watatoa ushirikiano ,muelewe huu mpango ni muhimu kwa serikali hivyo mkautekeleze kwa vitendo,serikali imewagharamia mje mjifunze ili kuwaelimisha wananchi na kuwa na maendeleo ya pamoja ngazi ya msngi na taifa, “amesema

Mbali na hayo amewataka washiriki hao kuwa makini na mijadala na kuachaa na matumizi ya simu bila mpangilio na kusisitiza kuwa Serikali imetumia gharama kubwa kuendesha mfunzo hayo hivyo ni wajibu wao kushiki kikamilifu.

Kwa upande wake Mkurugenzi idara ya maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na makundi maalum Bw.Patrick Golwike amewaelekeza wataalam hao kutumia nafasi hiyo kujifunza namna ya kuwahudumia wananchi ili kufikia maendeleo yaliyokusudiwa.

Amesema,”wananchi wanapenda huduma bora,na huduma hiyo inatokana na ninyi kuwa watendaji wazuri,wakiipenda huduma inamaanisha wanaipenda serikali yao, wakiichukia Serikali ni sisi ndiyo sababu,ili kufanikiwa lazima uzalendo na maadili yakawe nguzo kuu hatuna sababu ya kufanya kazi bila ushirikiano,’’amesisitiza na kuongeza kuwa ,

Kuna watu wapo hapa ni watendaji lakini wakikuta wananchi wanalalamika kuhusu kukosa huduma bora na wao pia wanalalamika wakati wao ni sehemu ya serikali, mnapaswa kuisemea serikali mambo mazuri na kuzingatia kutatua kero za wananchi kenye ngazi ya msingi,’’ameeleza.

About the author

mzalendoeditor