Featured Kitaifa

NAIBU WAZIRI MWANAIDI AHIMIZA UANZISHWAJI NA UENDELEZAJI WA DAWATI LA JINSIA LA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA MAENEO YA WAZI.

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaid Ali Khamis,akizungumza wakati akifungua warsha ya wadau wa Madawati ya kutokomeza vitendo vya Ukatili maeneo ya Umma yanaanzishwa na kuratibiwa katika uendeshaji wake iliyofanyika leo Oktoba 04, 2023 mjini Morogoro .

Na WMJJWM, Morogoro
 
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaid Ali Khamis, amewataka watendaji wa Serikali na wadau kuhakikisha Madawati ya kutokomeza vitendo vya Ukatili maeneo ya Umma yanaanzishwa na kuratibiwa katika uendeshaji wake.

Naibu Waziri Mwanaidi ameyasema hayo wakati akifungua Warsha hiyo ya Siku moja, Oktoba 04, 2023 mjini Morogoro iliyoshirikisha washiriki 50 kupitishwa katika Mwongozo wa Uanzishaji na Uendeshaji wa Dawati la kutokomeza vitendo vya Ukatili maeneo ya Umma.

Naibu Waziri Mwanaidi ameeleza kuwa washiriki wanatakiwa kuhakikisha wanauelewa vizuri Mwongozo huo ili waweze kwenda kuutekeleza kama shabaha ya Serikali inavyokusudia kuondoka na vitendo vya ukatili. 
 
Aidha Naibu Waziri Mwanaidi amesema kwa muda mrefu maeneo hayo yalikuwa hayana Mwongozo na hivyo kuyafanya maeneo hayo kuwa na vitendo vya ukatili vilivyosahamiri na watu kudhalilishwa bila sababu za msingi.
 
“Kwakuwa leo tupo kwenye mafunzo, nawasihi tupitie vizuri Mwongozo huu ambao utawezesha kuanzishwa kwa madawati hayo ambayo yatakuwa ni muarobaini wa kushughulikia masuala ya Ukatili wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake kwenye maeneo yaliyolengwa” amesema Naibu Waziri Mwanaidi.
 
Awali akimkaribisha kufungua mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Rennie Gondwe amesema mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo ya awamu ya kwanza ambayo yalifanyika kwa mwezi Februari 2023 ambapo jumla ya masoko 104 yamefanikiwa kuanzisha Dawati la Jinsia katika maeneo ya Masoko na kushughulikia matukio mbalimbali ya Ukatili wa Kijinsia.
 
“Mwongozo huu ulizinduliwa mkoani Kilimanjaro na Mhe. Waziri na mara baada ya uzinduzi yalifanyika mafunzo katika Mikoa sita ambayo Mwanza, Shinyanga, Geita, Arusha, Tanga na Kilimanjaro. Aidha, Waratibu 215 kutoka katika Halmashauri 43 za Mikoa tajwa wamesha patiwa mafunzo” amesema Gondwe.
  

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaid Ali Khamis (hayupo pichani)  wakati akifungua warsha ya wadau wa Madawati ya kutokomeza vitendo vya Ukatili maeneo ya Umma yanaanzishwa na kuratibiwa katika uendeshaji wake iliyofanyika leo Oktoba 04, 2023 mjini Morogoro .


 

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaid Ali Khamis,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua warsha ya wadau wa Madawati ya kutokomeza vitendo vya Ukatili maeneo ya Umma yanaanzishwa na kuratibiwa katika uendeshaji wake iliyofanyika leo Oktoba 04, 2023 mjini Morogoro .

About the author

mzalendoeditor