Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe. Jerry Silaa ,akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya makazi duniani leo Oktoba 2,2023 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda ,akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya makazi duniani leo Oktoba 2,2023 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhandisi Anthony Sanga
,akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya makazi duniani leo Oktoba 2,2023 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar Dkt. Mngereza Mzee Miraji,akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya makazi duniani leo Oktoba 2,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe. Jerry Silaa (hayupo pichani),wakati wa maadhimisho ya siku ya makazi duniani leo Oktoba 2,2023 jijini Dodoma.
Na Dotto Kwilasa, Dodoma
Serikali imesema ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha maboresho ya sera ya ardhi ambayo italeta suluhisho kwenye suala la umiliki wa ardhi ikiwa ni pamoja na kuwashughulikia wamiliki wasioendeleza ardhi.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya makazi duniani leo October 2,2023 Jijini hapa, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Jerry Silaa amesema Tanzania ikiwa inaadhimisha siku ya Makazi Duniani
bado kumekuwepo na changamoto ya migogoro ya Ardhi ya hapa na pale na kusababisha baadhi ya shughuli za uchumi kukwama kuendelea.
Amesema kwa kulitambua hilo Serikali inatumia siku hiyo kutafakari namna bora ya kuboresha hali ya makazi Katika miji na kuondokana na migogoro iliyopo.
Amesema,”Maadhimisho haya ni fursa Kwa wananchi na wadau wengine wa makazi kutafakari Kila mmoja namna anavyoshiriki kuboresha hali ya makazi na kutafakari ya kina kuhusu namna miji inavyoweza kukabiliana zinazoathiri uchumi,”amesema
Amesema lengo la Wizara ni kutoa huduma ya ugawaji viwanja viinavyoendana na huduma za jamii na kwamba matarajio hayo yatafufua uchumi wa pamoja.
Amesema Serikali itahakikisha inakuwa na mipango endelevu kwenye Sekta hiyo ili kukuza uchumi wa miji yenye tija na jumuishi ikiwa ni pamoja na kuwekeza miji endelevu ili kukuza nishati safi kulinda mifumo ikolojia.
“Tutaondokana na changamoto kwenye Sekta ya ardhi Kwa kuwezesha usanifu wa miji endelevu na mifumo mizuri ya utawala na makazi yenye mpangilio mzuri wa utawala wa ngazi mbalimbali ili kukuza biashara na utoaji huduma Kwa jamii,”amesema
Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Anthony Sanga amesema Wizara inajipanga kufanikiwa kuondoa kero ya uvamizi holela na kwamba kama vizara tayari wamefanya tathmini kuainisha maeneo ya kutilia mkazo zaidi ikiwemo upimaji bora wa ardhi .