Featured Kitaifa

BMH KUFANYA UPASUAJI MISHIPA YA DAMU YA UBONGO BILA KUFUNGUA FUVU

Written by mzalendoeditor

 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa(BMH)  Dkt. Alphonce Chandika,aakitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ushirikiano na wadau kutoka nchini Japan wa kutoa huduma ya upasuaji wa mishipa ya damu ya ubongo bila ya kufunua fuvu kwa kutumia mtambo maalum unaotumia teknolojia ya kisasa cha Anjo suti (Angio suit) leo Oktoba 2,2023 jijini Dodoma.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa(BMH)  Dkt. Alphonce Chandika,akifafanua jambo kwa  waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea ushirikiano na wadau kutoka nchini Japan wa kutoa huduma ya upasuaji wa mishipa ya damu ya ubongo bila ya kufunua fuvu kwa kutumia mtambo maalum unaotumia teknolojia ya kisasa cha Anjo suti (Angio suit) leo Oktoba 2,2023 jijini Dodoma.

Mtaalamu wa Afya kutoka TOKUSHUKAI Medical Group Prof. Hyodo Akio,akizungumza mara baada ya kuingia makubaliano na  Hospitali ya Benjamini Mkapa(BMH) kutoa huduma ya upasuaji wa mishipa ya damu ya ubongo bila ya kufunua fuvu kwa kutumia mtambo maalum unaotumia teknolojia ya kisasa cha Anjo suti (Angio suit) leo Oktoba 2,2023 jijini Dodoma.

Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mifupa ya Fahamu,Uti wa Mgongo na Ubongo kutoka BMH Henry Humba,akielezea jinsi utoaji  huduma ya upasuaji wa mishipa ya damu ya ubongo bila ya kufunua fuvu kwa kutumia mtambo maalum unaotumia teknolojia ya kisasa cha Anjo suti (Angio suit) leo Oktoba 2,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

HOSPITALI ya Benjamini Mkapa(BMH) imeingia ushirikiano na wadau kutoka nchini Japan wa kutoa huduma ya upasuaji wa mishipa ya damu ya ubongo bila ya kufunua fuvu kwa kutumia mtambo maalum unaotumia teknolojia ya kisasa cha Anjo suti (Angio suit).

Huduma hiyo inatajwa kupunguza gharama za matibabu na muda wa kuuguza Kidonda na muda wa daktari kufanya upasuaji.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 2,2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa BMH Dkt. Alphonce Chandika amesema wameingia ushirikiano huo ili kuendana na azma ya serikali ya kufungua mipaka na kuruhusu kushirikiana na wataalamu kutoka nje ambao wapo mbele kwa teknolojia ya matibabu.

”Huduma hiyo inatarajia kuanza ndani ya mwaka mmoja kwa sababu vifaa vipo,ikiwemo Madaktari bingwa wapo katika mafunzo yanayotolewa kwa ushirikiano wa Madaktari kutoka nchini Japani.”amesema Dkt.Chandika

BMH Hospital imekuwa ikishirikiana vizuri na TOKUSHUKAI Medical Group katika tiba ya upandikizaji figo,baada ya mafanikio kuonekana wameanza kushirikiana katika uanzishwaji wa utoaji huduma ya upasuaji ubongo bila kufungua fuvu.

“Tunaishkuru serikali kwa kuruhusu ushirikiano na hospitali za nje katika utoaji huduma za Afya ambazo hazipo nchini hii itasaidia kuongeza utalii wa matibabu,”amesem Dk Chandika.

Pia amesema kuwa  wajapani wametoa kifaa cha Anglesut ambacho hutumika katika upasuaji wa Ubongo bila kutumia fuvu.

“Tunawashkuru sana Prof. Hyodo Akio ambaye ni bingwa mbobezi na mshauuri wa huduma za Upasuaji Mishipa ya Damu ya Ubongo bila kufungua fuvu kutoka Japan na wenzake kwa ushirikiano wanatoa BMH ili kuhakikisha huduma hiyo inaanza,”amesema Dk Chandika.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mifupa ya Fahamu,Uti wa Mgongo na Ubongo kutoka BMH Henry Humba amesema tatizo la kiharusi ni kubwa na ni imani yao kuwa ndani ya mwaka mmoja huduma hiyo itaanza kutolewa.

“Kutumia teknolojia ya kisasa katika upasuaji wa Ubongo bila kufungua fuvu ina gharama nafuu kuliko mgonjwa kulazwa wodini,kwa sababu tiba hii inakwenda kuzibua mishipa ya Damu moja kwa moja,”amesema  Dk.Humba.

Amesema  huduma hiyo itaanza kutolewa katika hospitali ya Benjamin Mkapa ndani ya mwaka mmoja,baada ya Madaktari hao kupata Mafunzo.

” “Tutaanza kwa mjadala wa kitaaluma utakaolenga kutathimini hali halisi ya utoaji wa huduma za Upasuji wa Mifumo ya Fahamu, Uti wa Mgongo na Ubongo nchini kulekea kwenye ujuzi wa juu wa utoaji wa huduma hizo”amesema Dk Humba.

Amesema kuwa Mafunzo hayo yatakayodumu kwa siku tano mtawalia, yataongozwa na madaktari bingwa wabobezi wa Upasuaji wa Mishipa ya Damu ya Ubongo bila kufungua Fuvu kutoka nchini Japan na watashiriki kufanya Upasuaji na madaktari wazawa ikiwa ni hatua za awali kuwezesha huduma hizo nchini.

“Serikali ilikwisha leta vifaa ikiwemo mashine ya kuwezesha kufanyika kwa upasuaji, ikiwa na baadhi ya vifaa vinavyohitajika, kwa hiyo mafunzo haya ni hatua muhimu sana kwetu tunapoelekea kutumia mbinu hizo kutoa huduma” amesema Dkt. Humba.

Hata hivyo amesema kuwa serikali iko katika hatua za uanzishwaji wa vyumba vya stroke unit,ambapo serikali huwashirikisha Madaktari hao na kuongeza kuwa vyumba hivyo vitachangia kuongeza uharaka wa kuanzishwa kwa huduma hiyo.

Hospitali ya Benjamini Mkapa imeanzishwa kwa lengo la kutoa huduma za kibingwa na huduma bobevu ili kubeba dhima ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwawezesha wananchi wapate huduma iliyobora pasipo kusafiri kwenda nje kupata huduma ya matibabu.

About the author

mzalendoeditor