Featured Kitaifa

MWANDISHI MATHIAS CANAL ACHANGIA MIL 4 SHULE YA MSINGI KIOMBOI BOMANI WILAYANI IRAMBA

Written by mzalendoeditor

Na Mwandishi Wetu, Iramba-Singida

Mwandishi wa Habari Ndg Mathias Canal amechangia madawati 30 yenye thamani ya shilingi 2,100,000, na Vitakasa mikono 20 vyenye thamani ya shilingi 1,400,000.

Ametoa mchango huo leo tarehe 29 Septemba 2023 wakati akizungumza kwenye mahafali ya 60 ya shule ya msingi Kiomboi Bomani iliyopo katika kata ya Kiomboi, Wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Pamoja na mambo mengine pia Ndg Mathias amechangia kwa kutoa motisha ya shilingi 500,000 kwa ajili ya walimu katika shule hiyo kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ya kuwafundisha wananfunzi shuleni hapo.

Kadhalika amesema kuwa atawasomesha Watoto wote watakaomaliza darasa la saba na kupata ufaulu wa alama ‘’A’’ kwa kila somo kuanzia wale waliohitimu mwaka huu 2023 katika shule hiyo.

Katika hatua nyingine amewapongeza wazazi na walezi wa wanafunzi shuleni hapo kwa kukubali kuchangia kwa hiari baadhi ya mahitaji ya wanafunzi ikiwemo chakula kwa ajili ya wanafunzi ambao wapo katika madarasa ya mitihani.

Ameongeza kuwa wanafunzi hao bado hawajamaliza elimu ya darasa la saba mpaka pale watakapopata matokeo ya mitihani waliyoifanya hivyo wazazi na walenzi wanapaswa kuendelea kuimarisha ulinzi na mwenendo bora wa malezi kwa Watoto hao.

Pia Mwandishi Mathias Canal ameipongeza serikali kwa kutoa shilingi Mil 40 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa Pamoja na ofisi ya walimu.

Katika mahafali hayo Mwandishi Mathias Canal aliambatana na Diwani wa kata ya Kiomboi Mhe Omary Omary, na Mkurugenzi wa DM PLANET Ndg David Mtengile ambaye amechangia 100,000 kwa ajili ya motisha kwa walimu.

About the author

mzalendoeditor