Featured Kitaifa

WAZIRI WA UJENZI, MAWASILIANO NA UJENZI AWATAKA WANANCHI KUNUSURU MAZINGIRA YA BAHARI

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dkt. Khalid Mohamed akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba (hawapo pichani), wakati wa Maadhimisho ya Siku ya bahari iliyofanyika Kitaifa Mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Bi. Salama Mbarouk akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba (hawapo pichani), wakati wa Maadhimisho ya Siku ya bahari iliyofanyika Kitaifa Mkoani humo.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dkt. Khalid Mohamed akimsikiliza Mwanachama wa Taasisi ya Wanawake wanaofanya kazi katika sekta ya Usafirishaji Majini kwa Ukanda wa Masharii na Kusini mwa Bara la Afrika (WOMESA), Bi. Raya Khalfan, kuhusu shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo wakati Waziri huo alipotembelea banda la taasisi hizyo katika  Maadhimisho ya Siku ya bahari iliyofanyika Kitaifa Mkoani humo.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dkt. Khalid Mohamed akizungumza na viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika  Maadhimisho ya Siku ya bahari iliyofanyika Kitaifa Mkoani humo.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dkt. Khalid Mohamed (katikati waliokaa) katika pichaya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Uchukuzi na WIzara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi pamoja na taasisi za wizara hizo mara baada ya kufunga Maadhimisho ya Siku ya bahari yaliyofanyika Kitaifa Mkoani humo.

PICHA NA WIZARA YA UCHUKUZI

……..

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dkt. Khalid Mohamed amewataka wananchi wanaokaa katika visiwa vya Unguja na Pemba kutumia elimu ya masuala ya bahari kunusuru changamoto zinazoweza kujitokeza kwa matumizi mabaya ya bahari na rasilimali bahari.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya bahari ambayo kitaifa yamefanyika Mkoa wa Kusini Pemba Waziri Dkt. Mohamed amesema kwa miaka mingi wakazi wanaoishi katika visiwa hivyo wamekuwa wanufaika wa moja kwa moja kupitia bahari hivyo kwa kuitumia fursa hiyo vizuri kutawanufaisha kizazi cha sasa na badae.

“Takwimu zinaonyesha kuna idadi kubwa sana ya wavuvi, kina mama wanaojishughulisha na biashara ya mwani na majongoo, wote hawa wako kwenye bahari na wananufaika wao na familia zao hivyo lazima tuzingatie sana yale tuliyoelezwa na wataalam ili kuendelea kupata kipato kupitia bahari inayotuzunguka’ amesema Waziri Dkt. Mohamed.

Waziri Dkt. Mohamed amelipongeza Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC) na Shirika la Meli la Zanzibar (ZMA) kwa kuhakikisha wataalam wote wanakuwepo kutoa elimu ya ulinzi, usalama wa matumizi ya bahari ili kuwapa nafasi wananchi kupata uelewa mpana wa masuala yote yanayohusu bahari.

Aidha, Waziri Dkt. Mohamed ameongeza kuwa kwenye miundombinu ya Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi inaendelea kutekeleza miradi yake ya maboresho ya bandari ya Wete, shumba na Mkoani ili kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo kati ya Pemba na Tanga hadi Mombasa. 

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira Wizara ya Uchukuzi Bi. Stella Katondo amemuhakikishia Waziri Dkt. Mohamed kuwa Serikali zote zitaendelea kushirikiana kutoa elimu na kuandaa wataalam ambao watakuwa sehemu ya mabadiliko katika sekta ndogo ya bahari nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa ZMA, Sheikha  Mohamed amesema ZMA itaendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya bahari ili kuhakikisha rasilimali zilizopo zinatumika kwa kizazi cha sasa na badae huku zikikuza kipato cha Serikali na jamii kwa ujumla.

Maadhimisho ya Siku ya Bahari kwa mwaka huu yamefanyika kitaifa Mkoa wa Kusini Pemba ambapo yamefanywa sambamba na maonyesho na shughuli mbalimbali za ugawaji wa vifaa vya uokozi kwa wadau kuanzia 25 Septemba mpaka 28 Septemba 2023.

About the author

mzalendoeditor