Featured

SMZ,SMT KUSHIRIKIANA KATIKA TEHAMA

Written by mzalendoeditor

Na. Mwandishi Wetu

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi zanzibar (SMZ) Kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Serikali ya Muungano wa Tanzania (SMT) imeandaa Mkutano wa Wadau kuhusu Tamko la Amri ya Waziri kuhusu Critical Information Infrastructure (CII) na miongozo yake pamoja na mapendekezo ya uridhiwaji wa Mkataba wa Malabo Inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Bima Zanzibar, 29-30 Septemba, 2023.

Ndg, Mahfoudh Mohamed Hassan Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi amefungua Mkutano huo Kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, ameeleza kuwa Warsha hii inawaleta pamoja Wadau muhimu sana katika Sekta ya TEHAMA Kwa ajili ya kupata uelewa wa pamoja na baadae kukusanya maoni Kwa upande wa Zanzibar .

Aidha, amewaeleza Wajumbe kuwa chimbuko la Miundombinu Muhimu ya TEHAMA na Miongozo yake linatokana na hitaji la kutekeleza Sheria ya Makosa ya Mtandao ( Cybercrimes Act ) ya mwaka 2015 katika Kifungu Cha 28 ambacho kinampa Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana na Mawasiliano uwezo wa Kutambua na Kutangaza Miundombinu muhimu ya TEHEMA (Critical Information Infrastructure – CII) pamoja na miongozo yake. Lengo la kuwepo Kwa Kifungu hiki katika Sheria tajwa ni kuweka nguvu za Kisheria za utambuzi wa Miundombinu muhimu ya TEHAMA Nchini Ili iweze kupewa ulinzi mkubwa na kuhakikisha kuwa huduma za msingi kwa Wananchi zinapatikana.

‘ Niwaombe sote tushiriki Katika uelimishaji huu kwa makini Ili kuwezesha utoaji wa maoni katika Rasimu ya Tamko la Amri ya Waziri kuhusu Miundombinu muhimu ya TEHAMA na katika mapendekezo ya Uridhiwaji wa Mkataba wa Malabo Ili kuwezesha Wizara zetu kutimiza wajibu katika ujenzi wa Taifa letu’

Mkutano huu umehudhuriwa na

Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Wakuu wa Taasisi Chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Viongozi wengine kutoka Taasisi za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Wawezeshaji na Watumishi kutoka Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, pamoja na Waandishi wa Habari .

About the author

mzalendoeditor