Featured Kitaifa

TTCL MMEKABIDHIWA DHAMANA KUBWA YA KUILETEA NCHI MAENDELEO KUPITIA SEKTA YA MAWASILIANO-SHOMARI

Written by mzalendoeditor

 

 

Na Mwandishi wetu – Zanzibar
 
Mikakati mbalimbali inayotekelezwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) imesaidia kuimarisha biashara, kuinua uchumi na kuimarisha hali ya usalama wa nchi.
 
 
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Shomari Omari Shomari ,Septemba 23,2023 Visiwani Zanzibar wakati akifunga kikao kazi Cha Bodi ya wakurugenzi na Menejimenti ya TTCL chenye lengo la kufanya tathmini ya utendaji kazi kwa kuzingatia maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla.
 
” Naamini Mwenyekiti wa Bodi pamoja na Wajumbe na Menejimenti mtafanyaka usiku na mchana kuhakikisha matarajio ya serikali ya kuliona shirika hili linakuwa nyenzo muhimu katika kuifikia Tanzania ya Kidigitali yanafikiwa kikamilifu,”

 

 

Na kuongeza kuwa “Kikao hiki mlichokifanya leo ni muhimu sana katika kupelekea mustakabali mzuri wa Shirika letu, tukizingatia mabadiliko ya kibiashara (business transformation) ili kukidhi mahitaji ya jamii ambapo mawasiliano yamekuwa si anasa bali nyenzo muhimu ya kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali ikiwemo elimu mtandao, afya mtandao na huduma za kifedha kupitia simu za mkononi,”Amesema Shomari
 
Amewataka watumishi wa Shirika hilo kutumia vyema maarifa na uelewa wa mambo mbalimbali ya kimkakati, kisheria na kisera walivyovipata katika kikao kazi hicho kama nguzo muhimu na msaada mkubwa wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kama Viongozi na Wasimamizi wa shirika ili liweze kusonga mbele.
 
“Sisi wote tunataka kuiona TTCL ikipiga hatua katika maeneo ya kibiashara, utendaji wa kazi, pamoja na kubadilisha teknolojia. Soko la mawasiliano kwa sasa linachangamoto nyingi ambapo kila mmoja kwenye soko anabuni mkakati, teknolojia na bidhaa zenye kulenga kupata wateja wapya na kupanua wigo wa biashara kwa kila hali,”amesema Shomari
 
Pia amesisitiza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeipa dhamana kubwa Shirika hilo la kusimamia miundombinu ya mawasiliano,hivyo libebe maono makubwa ya Serikali ya kuifikisha Tanzania ya Kidigitali inafanikiwa na inaleta matunda.
 
 
Hivyo kuwataka watumishi wa TTCL kufanya kazi kwa bidii, weledi na kwa kutanguliza uzalendo,kwani Tanzania ya Kidigitali iko mikononi mwao.

 

About the author

mzalendoeditor