Featured Kitaifa

CHADEMA YAZIDI KUMEGUKA SINGIDA MASHARIKI

Written by mzalendoeditor

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM),Wilaya ya Ikungi kimevuna viongozi wa Baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(BAWACHA) kutoka Kata ya Makiungu na wanachama wengine 14 waliomua kujiunga na CCM kutokana na kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Raisi Mh Dr Samia Suluhu Hassan.

Wanachama hao wamerudisha kadi na kupewa kadi za CCM Septemba 21,2023,wakati wa hafla ya ugawaji wa majiko ya gesi 162 kwa wajasiriamali ikiwa ni mpango wa serikali chini ya Rais Samia wa kuwawezesha akina mama kiuchumi.

Wanachama hao wajasiriamali wanawake baada ya kuamua kujiunga na CCM,walikabidhiwa kadi za Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT),na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Mika Likapakapa kama ishara ya kuwapokea.

About the author

mzalendoeditor