Featured Kitaifa

SERIKALI KUENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WATAALAMU WA USTAWI WA JAMII

Written by mzalendoeditor

Na WMJJWM- Mwanza

Serikali imeahidi kuendelea kuwajengea uwezo wataalam wake ili waweze kuzingatia Uwiano wa Kijinsia na Ujumuishi Jamii katika Huduma za Ustawi wa Jamii

Hayo yamesemwa na Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Tullo Masanja, wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa wataalam 35 kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum pamoja na OR TAMISEMI yaliyofanyika Jijijini Mwanza.

Masanja amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea ujuzi wataalam wa Ustawi wa Jamii kuzingatia mahitaji ya makundi ya wanajamii yaliyo katika mazingira hatarishi.

Ameongeza kuwa wakati wa uandaaji wa Sera, Sheria, Kanuni, Mikakati na Mipango mbalimbali ya kijamii, ni muhimi kuzingatia matakwa ya makundi hayo ili kufikia malengo ya Nchi ya kizazi chenye usawa.

“Nazielekeza Halmashauri na Mkoa yote kwa kushirikiana kufanya utambuzi wa watu wanaoishi katika mazingira hatarishi na kutunza rejista yao kushirikiana na sekta zote kutoa huduma kwa wahitaji, kufanya tathminikwa wahitaji na kufanya tathmini na kuwapa huduma stahiki” alisema Masanja.

Mafunzo hayo yamehusisha Wataalam kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum , Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mikoa ya Kagera, Tabora, Shinyanga na Mwanza.

About the author

mzalendoeditor