Featured Kitaifa

ASKARI DODOMA WAKUMBUSHWA WAJIBU WAO

Written by mzalendoeditor

Jeshi la Polisi kupitia Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu  Septemba 19, 2023 limefanya Semina ya siku moja kwa Maafisa,wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wapatao (300) wa Mkoa wa Dodoma na Vikosi katika ukumbi wa Polisi Jamii Jijini Dodoma kwa lengo la kukumbushana na kujengeana uwezo kuhusu maswala Kuzuia na kushughlikia vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto.

Pia washiriki walikumbushwa maswala ya yahusuyo Ushilikishwaji wa jamii katika kubaini, kuzuia na kutanzua changamoto mbalimbali za uhalifu zikiwemo za maadili katika jamii pamoja na kuwahamasisha maafisa, wakaguzi na askari hao kufanya kazi kwa kuzingatia Nidhamu, Haki,Weledi na Uadilifu kwa kujenga taswira njema ya Jeshi la Polisi na kulifanya Jeshi la hilo kuaminika na Jamii.

Aidha, katika mafunzo hayo Mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto kutoka makao makuu ya Polisi Kamisheni ya Polisi Jamii Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Faidha Suleiman aliwataka askari kujitambua na kuacha tabia zote za ukatili na udhalilishaji wa Kijinsia katika familia zao na kuwasisitiza kufuata sheria za nchi hasa katika mahusiano.

Naye, Mkuu wa Kitengo cha Michezo Makao Makuu ya Polisi kutoka kamisheni ya Polisi jamii Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Jonas Mahanga aliwahimiza Polisi kata kutumia michezo katika kuwaunganisha vijana.

Picha na Benedict Mlawa wa Jeshi la Polisi

About the author

mzalendoeditor