Featured Kitaifa

RAIS DKT. MWINYI AZINDUA UBALOZI WA TANZANIA CUBA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.  Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa wakizindua Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Havana nchini Cuba katika hafla maalum iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.  Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Messa wakikata utepe wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Cuba iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.  Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano nchini Cuba kwa ajili ya kuzindua  Ubalozi huo katika hafla iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023 kulia kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Cuba Mhe. Humphrey Polepole na kushoto ni Mke wa Mhe. Dkt. Mwinyi Mama Mariam Mwinyi 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Havana nchini Cuba wakati wa hafla ya uzinduzi wa ubalozi huo iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.  Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua  Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano nchini Cuba  iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Messa akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua  Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano nchini Cuba  iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023 

…….

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.  Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezindua Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Havana nchini Cuba katika hafla maalum iliyofanyika jijini Havana tarehe 14 Septemba 2023.

Akizungumza katika uzinduzi wa Ubalozi huo Mhe. Rais Dkt. Mwinyi amesema kufunguliwa liwa kwa Ubalozi huo mwaka 2019 kunaonesha nia ya Tanzania ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Cuba na kujibu kitendo cha Cuba ilipofungua Ubalozi wake nchini mwaka 1962.

“kufunguliwa kwa Ubalozi huu mwaka 2019 kunaonesha nia ya Tanzania ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Cuba na kujibu kitendo cha Cuba ilipofungua Ubalozi wake nchini mwaka 1962,” alisema Dkt. Mwinyi.

Amesema kufunguliwa kwa ubalozi huo mwaka 2019 kunarahisisha uratibu wa shughuli za nchi zetu katika kuimarisha ushirikiano wa maendeleo ya kijamii na kuwaletea maendeleo wananchi wa nchi hizo.

Dkt. Mwinyi ameishukuru Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba na Serikali ya Jamhuri ya Cuba kwa ushirikiano mkubwa ambao imekua ikiupatia Ubalozi wa Tanzania Havana tangu ulipoanzishwa mwaka 2019 hadi wakati huu kitu ambacho kimeuwezesha Ubalozi huo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namshukuru Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba na Serikali ya Jamhuri ya Cuba kwa ushirikiano mkubwa ambao imekua ikiupatia Ubalozi huu tangu mwaka 2019 ulipofunguliwa, kitendo hicho kimeuwezesha Ubalozi wetu kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi,” alisema Dkt. Mwinyi.

Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa Ubalozi huo Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa amesema Serikali ya Cuba inauthamini uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Tanzania na itaendelea kufanya hivyo kwani uhusiano uliopo ni wa kindugu na wa kihistoria na kufanya hivyo ni kuwaenzi waanzilishi wa mataifa hayo.

“Mhe. Rais na Wananchi wote wa Tanzania, Serikali ya Cuba inauthamini uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Tanzania na itaendelea kuuthmini, uhusiano wetu ni wa Kidndugu na wa kihistoria na kufanya hivi ni kuwaenzi waanzilishi wa mataifa yetu,” alisema Mhe. Mesa

Mhe Mesa amesema Cuba inaipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uamuzi wake wa kufungua Ubalozi nchini Cuba na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuuwezesha Ubalozi huo kufanya kazi na kufikia malengo ya kuanzishwa kwake.

Akizungumza awali Balozi wa Tanzania nchini Cuba Mhe. Humphrey Polepole amesema Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano wake na Cuba uhusiano ambao ni wa kindugu na hasa ikizingatiwa kuwa Cuba ilikuwa miongoni mwa nchi za kwanza kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Tanzania.

Amesema Cuba imeendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta ya Afya ambapo wamekuwa wakibadilishana wataalamu wa afya kuanzia miaka ya 1960 hadi nyakati hizi kwa ajili ya kusaidia jamii za kitanzania katika eneo hilo.

About the author

mzalendoeditor