Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi wa Mkuranga alipoenda kukagua eneo la Kipala Mpakani-Mwandege ambalo litakalotumika kujenga stendi itakayoitwa Samia Bus Terminal.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Kipala Mpakani-Mwandege Mkuranga kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa wananchi wa eneo hilo ambalo litakalotumika kujenga stendi itakayoitwa Samia Bus Terminal.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija Nasri Ali akimpitisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa katika mchoro unaoonesha ramani ya kituo cha mabasi kitakachojengwa Mkuranga katika eneo la Kipala Mpakani-Mwandege.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza jambo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega kabla ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo ambalo litakalotumika kujenga stendi itakayoitwa Samia Bus Terminal.
Sehemu ya wananchi walioudhuria mkutano wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa aliofanya alipoenda kukagua eneo la Kipala Mpakani-Mwandege ambalo litakalotumika kujenga stendi itakayoitwa Samia Bus Terminal.
OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa amemueleza Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo kuharakisha upatikanaji wa fedha kiasi cha Sh. bilioni 38 kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya Mkuranga itakayofungua fursa kwa wananchi wa mikoa ya kusini mwa Tanzania.
Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo Septemba 12, 2023 alipokuwa akikagua eneo la Kipala Mpakani, Kata ya Mwandege Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani litakalotumika kujenga stendi hiyo itakayoitwa ‘Samia Bus Terminal Mkuranga’.
“Nimekuja kukagua na kujionea eneo la ujenzi wa stendi hapa Mkuranga, niwapongeze kwa hatua ambazo mmeanza kuchukua kwa kutenga eneo ambalo Stendi itajengwa, namuelekeza Katibu Mkuu TAMISEMI kuhakikisha fedha hizi zinapatikana na zinaletwa hapa Mkuranga ili kujenga stendi hii itakayofungua fursa za uchumi, kuleta ajira na kutoa huduma bora ya usafiri wa Mikoa ya Kusini,”amesema.
Akizungumzia Jina ambalo wananchi wa Mkuranga wameliainisha kwa ajili ya Stendi hiyo kuwa ni SAMIA BUS TERMINAL amesema maoni hayo yatawasilishwa kwa Mamlaka ili akiridhia stendi itakapokamilika iweze kuitwa jina hilo lililopendekezwa na wananchi.
Naye, Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega amesema eneo hilo lina ukubwa wa ekari 49 na halina mgogoro wowote na wananchi wamelilinda kwa muda mrefu kwa ajili ya kujengwa stendi hiyo.
‘Sisi tuko tayari kutafuta wawekezaji kwa ajili ya ujenzi wa majengo makubwa karibu na stendi hiyo, nyumba za kulala wageni na biashara zingine ili Stendi hiyo ikikamika hapa Mkuranga pachangamke kibiashara’ alisisitiza Mhe. Ulega.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mhe. Khadija Hassanal amesema kwa kipindi kirefu wananchi wa Mkuranga wametaabika kwa kukosa stendi ya uhakika na kwamba eneo hilo litakapojengwa stendi itakuwa ya kisasa yenye maegesho ya mabasi, malori, maeneo kupumzikia abiria pamoja na eneo ya wajasiriamali wadogo.
Naye, mkazi wa Mkuranga Bw. Ubaya Salehe amesema kuwa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita unajali wananchi ndio maana unawapatia fedha kwa ajili ya kujenga kituo cha mabasi ambacho kitakuwa na tija kwa wakazi wa Mkuranga na wananchi wa mikoa ya kusini.