Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, akizungumza na ujumbe wa Tanzania wakati wa kikao cha kukamilisha mapitio ya taarifa zitakazowasilishwa na Tanzania, katika mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, akimsikiliza Balozi wa Tanzania Jamhuri ya Korea Kusini Mheshimiwa Togolani Mavura, alipokuwa akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali wakati wa kikao cha kukamilisha mapitio ya taarifa zitakazowasilishwa na Tanzania, katika mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Amina Shaaban(kushoto), akitoa maelezo kuhusiana na ushiriki wa Tanzania mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine 54 za Afrika kushiriki mkutano huo Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini.
Kamishna Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, akifafanua jambo wakati kikao cha kukamilisha mapitio ya taarifa zitakazowasilishwa na Tanzania, katika mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (Korea-Africa Economic Cooperation (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, akiongoza kikao cha ujumbe wa Tanzania kukamilisha mapitio ya taarifa zitakazowasilishwa katika mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini.