Featured Kitaifa

WAFANYABIASHARA MAWEZI WANOLEWA MATUMIZI YA MIZANI

Written by mzalendoeditor

NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO

Meneja wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) Mkoa wa Morogoro Fanuel Mtitu amewataka wafanyabiashara na wanunuzi kuzingatia matumizi sahihi ya vipimo ili kuweza kufikia uchumi wa kati.

Mtitu ameyasema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Mawezi Manispaa ya Morogoro ikiwa ni sehemu ya utoaji wa elimu juu ya matumizi ya mizani kwa wafanyabiashara wa soko hilo. 

Amesema mzani ni ndio kipimo pakee kinachoondoa malalamiko hivyo ni vyema kwa wafanyabiashara kuzingatia matumizi sahihi ya mizani ili kukuza uchumi wao nan chi kwa ujumla.

“Ukitumia mzani hakuna atakayekuomba umuongeze, eti umempunja, hakuna malalamiko hayo kwenye mizani. Mfanyabishara mzuri anatumia mzani katika biashara yako.” Alisema Meneja Wakala wa vipimo Mkoa wa Morogoro. 

Aidha wameataka wafanyabiashara kufika ofisini kwake pale wanapopata changamoto yeyote kwenye mizani wanayoitumia pia wanaponunua mizani wahakikishe imekaguliwa na wakala wa vipimo Tanzania kabla ya kuaanza kuitumia.

Kwa upande wao wafanyabiashara wa Soko la Mawezi akiwemo Seleman Rashid na Rajabu Hassan wamesema kuna baadhi ya bidhaa akitolea mfano wa Nyanya na Bamia wanapata changamoto ya kupima kwenye mzani, hivyo elimu walioipa itawasaidia kuwaelewesha wateja na kuweza kutumia mzania.

About the author

mzalendoeditor