Featured Kitaifa

SERIKALI ITAENDELEA KUMUENZI MAREHEMU MEMBE-MAJALIWA

Written by mzalendoeditor

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Ibada ya Kumbukumbu ya marehemu Bernard Membe iliyofanyika nyumbani kwa marehemu kijijini Londo katika Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi,

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mjane wa marehemu Bernard Membe , Dorcas Membe baada ya  Ibada ya  Kumbukumbu ya marehemu Bernard Membe  iliyofanyika nyumbani kwa marehemu kijijini  Londo katika Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Bernard Membe baada ya kushiriki Ibada ya Kumbukumbu ya marehemu Bernard Membe iliyofanyika nyumbani kwa marehemu kijijini  Londo katika Halmashauri ya Mtama mkoani Lindi,

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Bernard Membe baada ya kushiriki Ibada ya Kumbukumbu ya marehemu Bernard Membe iliyofanyika nyumbani  kwa marehemu kijijini Londo katika Halmashauri ya Mtama mkoani Lindi.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete na Mama Salima Kikwete wakiwa katika Ibada ya Kumkumbuka marehemu Bernard Membe iliyofanyika nyumbani kwa marehemu kijijini  Rondo katika Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuelekea kwenye kaburi la marehemu Bernard Membe  kwa ajili ya kuweka mashada ya maua baada ya kushiriki Ibada ya Kumbukumbu ya marehemu Bernard Membe iliyofanyika nyumbani kwa marehemu kijijini Londo katika Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi Agosti 26, 2023. Kulia ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Taknolojia ya Habari, Nape Nnauye na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi,  Hassan Jarufu na kushoto ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Richard Kasesela. (Picha naOfisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuyaenzi mambo yote mazuri yaliyofanywa na marehemu, Bernad Membe wakati wa utumishi wake Serikalini.

Marehemu Membe ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje alifariki dunia Mei 12 mwaka huu katika hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Amesema marehemu Membe enzi za uhai wake alikuwa mwanadiplomasia mahiri kwenye medani za Kitaifa na Kimataifa, hivyo Serikali na Watanzania wataendelea kumkumbuka.

Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Agosti 26, 2023) aliposhiriki ibada ya kumbukumbu ya marehemu Membe iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Rondo, Lindi.

Amesema weledi, nidhamu, uchapakazi na umahiri wa marehemu Membe uliitambulisha Tanzania katika medani za kimataifa na kutengeneza marafiki na mataifa mengine.

“Mheshimiwa Membe alikuwa na weledi wa kitaifa na kimataifa, jumuiya za kimataifa zinatambua umahiri wake  na alijizolea sifa kwa sababu ya nidhamu na uchapakazi wake.”

Naye, Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza kwa niaba ya familia ya marehemu aliishukuru Serikali kwa ushirikiano ilioutoa katika kipindi cha msiba.

“Namshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya ukarabati wa kanisa ulioanzishwa na marehemu Membe. “

About the author

mzalendoeditor