Featured Kitaifa

TUME YA TEHAMA KUJENGA VITUO VYA UBUNIFU KANDA TANO NCHINI

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama Dkt. Nkundwe Mwasaga,akizungumza na Waandishi wa habari leo Agosti 25,2023 jijini Dodoma  kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Tume hiyo na Mwelekeo wa Utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2023/24.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama Dkt. Nkundwe Mwasaga,akimsikiliza Mwandishi wa habari kutoka Uhuru FM Bi.Sakina Abdulmasoud akiuliza Swali leo Agosti 25,2023 jijini Dodoma  kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Tume hiyo na Mwelekeo wa Utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2023/24.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari-MAELEZO Bw.Gerson Msigwa,akizungumza mara baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama Dkt. Nkundwe Mwasaga,kutoa taarifa kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Tume hiyo na Mwelekeo wa Utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 leo Agosti 25,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

TUME ya Tehama (ICTC) imeanika vipaumbele 13 ikiwemo kukamilisha vituo vya ubunifu wa tehama kwa lengo la kuleta mapinduzi ya teknolojia na ubunifu nchini.

Hayo yamesemwa leo Agosti 25,2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama Dkt. Nkundwe Mwasaga,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Tume hiyo na Mwelekeo wa Utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2023/24.

Dkt.Mwasaga amesema Vituo hivyo vinatarajiwa kujengwa katika kanda tano nchini pamoja na kuanzisha kituo kimoja Zanzibar.

”Tunatarajia Kuanzisha kituo cha kutengeneza na kuboresha vifaa vya TEHAMA (ICT Refurbishment and Assembly centre) na vituo vya majaribio vya ubunifu TEHAMA (District ICT Startups Innovation hubs) katika Wilaya 10.”amesema Dkt.Mwasaga 

Hata hivyo amesema kuwa watafanya tafiti za maendeleo ya TEHAMA nchini na kufanya tathmini ya kitaifa ya hatua za utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya TEHAMA.

Pia wataratibu na kuandaa matukio ya kuvutia uwekezaji na kutangaza masoko ya bidhaa za TEHAMA ndani na nje ya nchi.

”Kushirikiana na washirika wa maendeleo na kampuni za kimataifa katika kuendeleza bunifu za TEHAMA ikiwemo kuwezesha utengenezaji wa bidhaa za TEHAMA hapa nchini.”amesema 

Amesema kuwa watajenga kituo cha Artificial Intelligence kwa ajili ya kuendeleza wataalam wa TEHAMA pamoja na Kuwezesha mafunzo maalum ya wataalam wa TEHAMA 500 ili kukuza na kuendeleza ujuzi wa TEHAMA nchini.

Aidha amesema wanatarajia Kukuza soko la bidhaa na huduma za kampuni ndogondogo “startup” kwa kushiriki maonesho na makongamano yanayohusu fursa za startups duniani.

”Kuratibu na kutengeneza mfumo wa usimamizi wa utekelezaji wa Sera ya TEHAMA na kufanya tafiti za kuweza kufanya maboresho ya sera kulingana na mabadiliko ya teknolojia.”amesema

Pia watajenga metaverse studio kwa ajili ya kutengeneza maudhui ya metaverse na pia kuboresha maudhui ya mitandao.

Amesema kuwa wanatarajia Kufanya tafiti za maendeleo ya TEHAMA kwa kila wilaya na Kuanzisha Kituo cha Resilience Academy hapa nchini.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari-MAELEZO Bw.Gerson Msigwa,amesema serikali imeamua kuwekeza kwa nguvu kwenye Tanzania ya kidigitali na Tume hiyo inasimamia azma hiyo.

“Kuna nchi uchumi wa kidigitali umewafikisha mbali sana kama Marekani masuala ya Tehama yanachangia kwa asilimia 10,”amesema Bw.Msigwa

About the author

mzalendoeditor