Featured Kitaifa

DC KIGOMA: EWURA WASIMAMIENI KIGOMA WSSA

Written by mzalendoeditor

 

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Mhe. Salum Kali, akizungumza wakati akifungua mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi (taftishi) kuhusu ombi la kurekebisha bei za huduma za Majisafi za Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Kigoma (WSSA)uliofanyika leo Agosti 25,2023.

Kaimu Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mha. Walter Christopher, akizungumza kwenye mkutano wa kukusanya maoni ya wadau (taftishi) kuhusu ombi la kurekebisha bei za huduma za majisafi na usafi wa mazingira Kigoma (WSSA), uliofanyika leo Agosti 25,2023.

Baadhi ya Wananchi wa Kigoma, wakifuatilia kwa makini mkutano huo

Baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Kigoma, wakitoa maoni yao kuhusu marekebisho ya bei za huduma za maji na usafi wa mazingira Kigoma.

Na.Mwandishi Wetu-KIGOMA
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Mhe. Salum Kali, ameitaka EWURA kuisimamia vizuri Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kigoma ili wananchi wa Kigoma wapate huduma ya majisafi kwa wakati na kwa bei sahihi.

Mhe. Kali ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi (taftishi) kuhusu ombi la kurekebisha bei za huduma za Majisafi za Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Kigoma leo Agosti 25,2023.

“Wasimamieni mamlaka ya maji vizuri ili wananchi wafurahie huduma ya maji nchini,” alisema
Mhe. Kali na kuongeza kuwa watumiaji wa huduma ya maji wana wajibu wa kutoa maoni kwa uwazi ili kuiwezesha Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Kigoma kutoa huduma bora.

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mha. Walter Geofrey alisema, EWURA hutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia uwazi, uwajibikaji, maamuzi yanayo tabirika na ushirikishaji wadau, hivyo mkutano huo umelenga kushirikisha wadau wa maji ili kupata maoni yao juu ya bei mpya za maji zinazopendekezwa.

About the author

mzalendoeditor