Featured Kitaifa

SHIRIKA LA CAMARA EDUCATION TANZANIA LIMETOA KOMPYUTA ZENYE THAMANI YA SH. MILIONI 37 KUPITIA TEA

Written by mzalendoeditor
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Bi. Jokate Mwegelo (kushoto) akipokea Kompyuta kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Utafutaji Raslimali na Usimamizi wa Miradi wa TEA, Bw. Masozi Nyirenda katika hafla ya kukabidhi msaada wa Kompyuta kwa ajili ya Shule ya Sekondari Semkiwa ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Shule ya Sekondari ya Kwaluguru ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni za Mkoani Tanga. Kila shule imepokea Kompyuta 25.
Shirika la Camara Education Tanzania limetoa msaada wa Kompyuta 100 zenye thamani ya Sh. Milioni 37 kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ambayo ina jukumu la kisheria la kukusanya michango kwa ajili ya sekta ya elimu nchini.
 
Kompyuta hizo 100 zimetolewa kwa shule nne za Sekondari zilizoko kwenye Mikoa ya Tanga na Pwani ambapo kila shule imepata Kompyuta 25 kwa lengo la kuwezesha wanafunzi kupata masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
 
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi kompyuta hizo iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Semkiwa Wilayani Korogwe Mkoani Tanga tarehe 23 Agosti 2023, Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Jokate Mwegelo amewahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii kutokana na kuwekewa mazingira mazuri ya kujifunza na kufundishia.
 
“Namna pekee mnyoweza kuonyesha shukrani kwa wafadhili walioleta msaada shuleni kwenu ni kusoma kwa bidii na kuendelea kufanya vizuri katika masomo yenu”. Amesema Mkuu wa Wilaya ya Korogwe.
 
Katika hafla hiyo, shule ya Sekondari Semkiwa ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Shule ya Sekondari Kwaluguru ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni zimekabidhiwa Kompyuta 25 kila moja.
 
Kwa upande wa Mkoa wa Pwani wanufaika ni Shule ya Sekondari Rafsanjani Soga iliyopo katika Halmashauri ya Mji Kibaha na Shule ya Sekondari Simbani iliyopo katika Halmashauri ya Kibaha ambapo kila shule itapata Kompyuta 25.
 
Mwakilishi wa Camara Education Tanzania, Bi. Asia Bonanga amesema shirika la Camara Education Tanzania, linajikita katika kupeleka teknolojia ya mawasiliano mashuleni ili kusaidia jitihada za kupatikana kwa elimu bora nchini.
 
Ameongeza kuwa maono ya Camara Education Tanzania ambalo ni kuona hakuna mwanafunzi anayeachwa nyuma katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano – TEHAMA.
 
Kaimu Mkurugenzi wa Miradi na Utafutaji Raslimali na Usimamizi wa Miradi kutoka TEA, Bw. Masozi Nyirenda ameshukuru Shirika la Camara Education Tanzania kwa msaada huo wa Kompyuta na kukumbusha shule zilizonufaika kuzitumia na kuzitunza vizuri ili zidumu na kunufaisha kundi kubwa la wanafunzi.
 
“Kama tunavyofahamu vifaa hivi vinahitaji utunzaji maalum ikiwa ni pamoja na kuwa na vyumba vinavyofaa, hivyo shule nufaika zijiandae vyema kwa hili” ameongeza Bw. Nyirenda.
 
 
 
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Bi. Jokate Mwegelo (kushoto) akimkabidhi Kompyuta Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Mhe. Fransis M. Komba katika hafla ya kukabidhi msaada wa Kompyuta kwa Shule ya Sekondari Semkiwa ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Shule ya Sekondari ya Kwaluguru ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni za Mkoani Tanga. Kila shule imepata kompyuta 25.
 
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Bi. Jokate Mwegelo akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uendeshaji wa Shirika la Camara Education Tanzania, Bw. Godfrey Ezekiel katika hafla ya kukabidhi msaada wa Kompyuta zilizotolewa na shirika la Camara Education Tanzania kupitia TEA kwa ajili ya Shule ya Sekondari Semkiwa ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Shule ya Sekondari ya Kwaluguru ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni za Mkoani Tanga.
 
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Bi. Jokate Mwegelo akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Semkiwa ambako amekuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya kukabidhi msaada wa Kompyuta katika shule hiyo na Shule ya Sekondari ya Kwaluguru ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni za Mkoani Tanga.
 
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Bi. Jokate Mwegelo (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Tito Mganwa katika hafla ya kukabidhi msaada wa Kompyuta zilizotolewa na shirika la Camara Education Tanzania kupitia TEA kwa Shule ya Sekondari Semkiwa iliyoko Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Shule ya Sekondari ya Kwaluguru ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni za Mkoani Tanga.
 
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Bi. Jokate Mwegelo akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa Kompyuta kwa Shule ya Sekondari Semkiwa na Shule ya Sekondari ya Kwaluguru za Mkoani Tanga. Msaada huo umetolewa na shirika la Camara Education Tanzania kupitia TEA.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Semkiwa wakitoa burudani ya ushairi katika hafla ya kukabidhi msaada wa Kompyuta kwa Shule ya Sekondari Semkiwa ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Shule ya ya Sekondari ya Kwaluguru ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni za Mkoani Tanga.

About the author

mzalendoeditor