Featured Kitaifa

WAZIRI KIJAJI ATETA NA WAFANYABIASHARA MKOA WA DODOMA 

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Viwanda na Biashara  Dkt. Ashatu Kijaji,akizungumza  wakati wa Kikao kazi na wafanyabiashara  wa jijini la  Dodoma,wajasiriamali na wafanyabiashara pamoja na majukwaa yanayojihusisha na ujasiriamali kilichofanyika jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Viwanda na Biashara  Dkt. Ashatu Kijaji amewataka wafanyabiashara wa Mkoa wa Dodoma kuchangamkia fursa zinazojitokeza kwa kujenga miundombinu wezeshi kwa wawekezaji na wageni  kwani baada ya Serikali kuhamia Jijini Dodoma kumekuwa na ongezeko la wageni kutoka sehemu mbalimbali Duniani.

Waziri Kijaji ameyasema hayo wakati wa Kikao kazi na wafanyabiashara wa Jiji la Dodoma  ambapo  kimewahusisha wajasiriamali na wafanyabiashara pamoja na majukwaa yanayojihusisha na ujasiriamali. 

Amesema uchumi imara wa Taifa upo mikononi wa sekta binafsi hivyo amewahimiza wafanyabiashara hao kutumia fursa zote zinazojitokeza iwe ni sekta binafsi au kutoka serikalini ili kuendelea kukuza uchumi wa nchi. 

Waziri Kijaji amewahimiza wajasiriamali kuwa waaminifu na Fedha zinazotolewa na Serikali kama sehemu ya mtaji ili kuwawezesha na wengine kupata hiyo fursa.

“Lazima tukubaliane na utaratibu uliowekwa uadilifu wetu, uaminifu wetu ni muhimu hakuna fedha za bure sehemu yeyote lazima uwe na uhakika wa fedha kurudi na mtu unae mpatia fedha hivyo tunatakiwa kumthibitishia Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama alivyo mtetezi wetu namba moja “amesema Dkt. Kijaji

Kwa Upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amempongeza Waziri Kijaji kwa kukutana na kuzungumza na wafanyabiashara hao pamoja na kutatua changamoto na kero zilizokuwa kikwazo katika utekelezaji wa biashara zao.

 ”Mkoa wa Dodoma upo tayari kupokea wawekezaji na kuongeza idadi ya viwanda ili kuongeza na kukuza mapato ya Serikali na uchumi wa nchi ya Tanzania.”amesema Mhe.Senyamule

 

WAZIRI wa Viwanda na Biashara  Dkt. Ashatu Kijaji,akizungumza  wakati wa Kikao kazi na wafanyabiashara  wa jijini la  Dodoma,wajasiriamali na wafanyabiashara pamoja na majukwaa yanayojihusisha na ujasiriamali kilichofanyika jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe,,akizungumza wakati wa Kikao kazi na wafanyabiashara  wa jijini la  Dodoma,wajasiriamali na wafanyabiashara pamoja na majukwaa yanayojihusisha na ujasiriamali kilichofanyika jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wake wakati wa Kikao kazi cha Waziri wa Viwanda na Biashara  Dkt. Ashatu Kijaji,na wafanyabiashara  wa jijini la  Dodoma,wajasiriamali na wafanyabiashara pamoja na majukwaa yanayojihusisha na ujasiriamali kilichofanyika jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri  wa Viwanda na Biashara  Dkt. Ashatu Kijaji,(hayupo pichani) akizungumza  wakati wa Kikao kazi na wafanyabiashara  wa jijini la  Dodoma,wajasiriamali na wafanyabiashara pamoja na majukwaa yanayojihusisha na ujasiriamali kilichofanyika jijini Dodoma.

Wafanyabiashara mbalimbali wakichangia hoja wakati wa Kikao kazi na wafanyabiashara  wa jijini la  Dodoma,wajasiriamali na wafanyabiashara pamoja na majukwaa yanayojihusisha na ujasiriamali na Waziri  wa Viwanda na Biashara  Dkt. Ashatu Kijaji.

About the author

mzalendoeditor