MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii usiku huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Mabao ya Yanga yote yamefungwa na washambuliaji wake, Stephane Aziz Ki dakika ya 85 na Clement John Mzize dakika ya 89.
Wawili hao wote walifunga baada ya kutokea benchi kwa pamoja dakika ya 62, Aziz Ki akichukua nafasi za Crispin Ngushi na Mzize nafasi ya Farid Mussa.
Yanga sasa imeingia Fainali ambayo itachezwa Jumapili na itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kesho baina ya Simba SC na Singida Fountain Gate hapo hapo Mkwakwani Saa 1:00 usiku.