Featured Kitaifa

SERIKALI KUKISAIDIA KIWANDA CHA KUTENGENEZA VIPURI KILIMANJARO

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji  amesema Serikali itahakikisha inakisaidia Kiwanda cha kutengeneza Vipuri Kilimanjaro ( KMTC) kufikia malengo katika masoko kwa kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuona uzalishaji wa ndani unafanyika kupitia chuma kinachozalishwa nchini.

Amesema hayo  alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Kilimanjaro kujionea shughuli zilipo  pamoja na kisikiliza na kutatua changamoto zao.

Aidha amewapongeza wafanyakazi wa kiwanda hicho na kuwataka  kuwa waaminifu kwa kuwa Serikali inafanya jitihada mbalimbali za kuweka mazingira bora ya biashara ili kuvutia wawekezaji katika viwanda vitakavyotumia vipuri vinavyotengenezwa na kiwanda hicho

   

About the author

mzalendoeditor