Muonekano wa sehemu ya tangi la Mradi wa maji Masengwa awamu ya pili kwa ajili ya vijiji vya Ishinabulandi na Bubale Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa akishuka kwenye tangi la Mradi wa maji Masengwa awamu ya pili kwa ajili ya vijiji vya Ishinabulandi na Bubale Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim ameweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili utakaonufaisha vijiji nane kata ya Masengwa, Mwamala na Samuye Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga unaotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) unaotarajiwa kunufaisha zaidi ya watu 24,252 ukigharimu shilingi 4,751,365,960.00
Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Abdalla Shaib Kaim ameweka jiwe la msingi la mradi huo leo Jumamosi Julai 29,2023 baada ya kukagua na kujiridhisha kuhusu ubora na gharama za mradi huo.
“Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 zimefika katika mradi huu, tumepokea taarifa ya mradi, Mwenge wa Uhuru umefanya ukaguzi wa kina kuhusu nyaraka zinazohusiana na mradi, umetembelea na kujionea miundombinu ujenzi ulipofikia. Tunafanya haya ili kuhakikisha tunabaini ubora na viwango vinavyotakiwa katika mradi husika, thamani ya pesa iliyotumika kama inaaksi maendeleo na uhalisia wa matokeo ya mradi. Lengo kuu ni kuhakikisha fedha zinazotolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mapenzi makubwa ya kuwaletea Watanzania maendeleo yanayolenga kuleta tija na afya kwa maslahi mapana ya Watanzania na siyo maslahi ya mtu binafsi”,amesema Kaimu.
“Baada ya ukaguzi wa kina ambao Mwenge wa Uhuru umefanya, kwanza kwa upande wa nyaraka, nyaraka tumejiridhisha zote ziko vizuri hongereni sana, mradi unaendelea vizuri, kazi kubwa kazi nzuri imefanyika. Tunaamini mradi huu unaenda kutimiza dira na maono ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo wananchi kwa kusogeza kwa ukaribu zaidi upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama na unalenga kumtua mama ndoo kichwani. Tunawashukuru RUWASA kwa kazi nzuri, hongereni sana. Tunaweka jiwe la msingi”,ameongeza Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim.
Akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa mradi huo, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Shinyanga, Emaeli Songelaeli Nkopi amesema mradi huo hadi kukamilika unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi 4,751,365,960.00 (Bila VAT) ambapo chanzo cha fedha hizo ni Serikali Kuu kupitia mfuko wa Maji wa Taifa (NWF).
“Lengo la mradi huu ni kutoa huduma ya maji kwa wananchi wa katika vijiji nane vya Ishinabulandi, Isela, Idodoma, Ibingo na Ng’wang’halanga (kata ya Samuye), Bubale (kata ya Masengwa) na Ibanza na Mwamala “B” (kata ya Mwamala)”,amesema Mhandisi Nkopi.
“Ujenzi wa mradi huu ulianza tarehe 25/02/2022 na unatarajia kukamilika tarehe 24/08/2023 na unatekelezwa na Mkandarasi mzawa Mbeso Construction Company wa Dar-es-Salaam. Mradi huu unahusisha ujenzi wa “off take” mbili, DP 46 za maji, matangi mawili ya maji (Ishinabuladi lita 100,000 na Mwamala lita 200,000), mtandao wa bomba za ukubwa tofauti kuanzia 32mm hadi 250mm wenye urefu wa km 71.82 na utasimamiwa na kuendeshwa na CBWSO”,ameeleza Mhandisi Nkopi.
Ameongeza kuwa mradi wa maji Masengwa II umetekelezwa kutokana na uhitaji wa huduma ya maji kwa wananchi, utekelezaji wa Sera ya Maji ya Mwaka 2002, utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Maji na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020-2025.
Mhandisi Nkopi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutekeleza mradi huu wa kimkakati ambao utawanufaisha zaidi ya watu 24,252.
Nao wakazi wa Ishinabulandi wameishukuru serikali kwa ujenzi wa mradi wa maji hali ambayo itawasogezea karibu huduma ya maji kwani wamekuwa wakitumia maji yasiyo salama na kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma ya maji.
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 ni “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa”.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim akikata utepe wakati akiweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo Jumamosi Julai 29,2023. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim akiweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA Kishapu, Neema Mwaifuge akisoma maandishi baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya tangi la Mradi wa maji Masengwa awamu ya pili kwa ajili ya vijiji vya Ishinabulandi na Bubale Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye tangi la Mradi wa maji Masengwa awamu ya pili kwa ajili ya vijiji vya Ishinabulandi na Bubale Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Shinyanga, Emaeli Songelaeli Nkopi (kulia) akielezea kuhusu Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Shinyanga, Emaeli Songelaeli Nkopi akielezea kuhusu Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Shinyanga, Emaeli Songelaeli Nkopi (katikati) akielezea kuhusu Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Shinyanga, Emaeli Songelaeli Nkopi akisoma taarifa ya ujenzi wa Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum akizungumza kwenye Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim akizungumza kwenye Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim akizungumza kwenye Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Mmoja wa wananchi akiishukuru serikali kwa kuwajengea Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Mmoja wa wananchi akiishukuru serikali kwa kuwajengea Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Mwenge wa Uhuru ukiondoka katika Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Wafanyakazi wa RUWASA wakipiga picha ya kumbukumbu katika Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Viongozi wa RUWASA wakipiga picha ya kumbukumbu katika Mradi wa Maji Masengwa awamu ya pili Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya tangi la Maji kwenye Mradi wa maji Masengwa awamu ya pili kwa ajili ya vijiji vya Ishinabulande (kata ya Masengwa) na Bubale (kata ya Samuye) Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.