Featured Kitaifa

WAFANYAKAZI WA HOTELINI WAPEWA MAFUNZO YA HUDUMA YA KWANZA

Written by mzalendoeditor

 

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Wafanyakazi 700 wa hotelini mkoani Arusha kupitia Programu ya Kukuza Ujuzi inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wamepewa mafunzo ya kutoa Huduma ya Kwanza, ili kutoa huduma bora kwa watalii wanaokuja nchini.

Mafunzo hayo yanayotekelezwa na ofisi hiyo ni miongoni mwa mikakati ya kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kupaisha sekta ya utalii nchini kwa kuhakikisha watalii wanahudumiwa kwa weledi na ujuzi stahiki.

Akitoa mafunzo ya huduma ya kwanza kwa wafanyakazi hayo, Mwezeshaji Dk.Christopher Nzella, amehimiza wafanyakazi hao kujua namna ya kuwahudumia watu waliopata mshtuko, kuzimia au tatizo lolote la ghafla ya kiafya.

“Ni muhimu kuwa na sanduku la huduma ya kwanza kwenye hoteli zenu kubwa hata nyumbani, mfano mgeni amekuja katoka porini amevimba unampeleka eneo la huduma ya kwanza unampa huduma stahiki, hii itasaidia hata wanaporudi kwenye nchi zao wanasema hatujawahi kutana na huduma bora kwenye hoteli fulani ya Tanzania,”amesema.

About the author

mzalendoeditor