Featured Kitaifa

SERIKALI KUANZISHA MFUMO WA KIELETRONIKI WA UKUSANYAJI TAARIFA WENYE ULEMAVU.

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa KItengo Cha wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu TEHAMA Bi. Fatma Mgembe (katikati) akiwa na Afisa Ustawi wa Jamii wa Ofisi hiyo Bw. Gerold Komba (kulia) na (kushoto) ni mratibu wa kipindi Cha Hello Tanzania Cha Radio Uhuru bi. Sakina Abdulmasoud wakati wa kutoa elimu Kwa umma.

Na; Mwandishi Wetu – DODOMA.

Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu inatarajia kuanzisha mfumo wa kielektroniki utakao wezesha kukusanya taarifa za watu wenye ulemavu.

Aidha,mfumo huo utawezesha kusajili, kuratibu, kusimamia na kufuatilia masuala na huduma zinazowahusu Watu wenye Ulemavu.

Hayo yamebainishwa tarehe 26 Julai, 2023 Jijini Dodoma na Mkuu wa kitengo cha TEHAMA Bi. Fatma Mgembe pamoja na Afisa Ustawi wa Jamii, Bw. Gerold Komba kutoka ofisi hiyo walipokua wakitoa elimu kwa umma kuhusu mfumo huo.

Wamesema lengo la kuanzishwa kwa mfumo huo utawezesha upatikanaji wa uhakika wa taarifa za Watu wenye Ulemavu, kutambua aina, mahitaji na idadi ya Watu wenye Ulemavu, kujua vyanzo vya Ulemavu na kuwa na mipango thabiti ya kuhudumia kundi la Watu wenye Ulemavu.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii, Bw. Gerold Komba amesema mfumo huo ni uboreshaji wa rejesta ya Watu wenye Ulemavu ili kuongeza ufanisi katika utendaji na uchambuzi wa taarifa za Watu wenye Ulemavu.

Aidha ametoa rai kwa wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa watendaji watakao kuwa wanakusanya taarifa hizo ili Watu wenye Ulemavu waweze kusajiliwa katika mfumo huo, utakao iwezesha serikali kutekeleza hatua endelevu kwa ustawi.

About the author

mzalendoeditor