Featured Kitaifa

WAFANYAKAZI WA HOTELINI WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAPA UJUZI

Written by mzalendoeditor

Na Mwandishi Wetu, Arusha
Wafanyakazi wa hotelini wameipongeza serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kuwapatia mafunzo ya kukuza ujuzi yatakayosaidia kutoa huduma bora kwa watalii.

Wakizungumza Julai 25, 2023 jijini Arusha kwenye mafunzo hayo yanayotolewa kwa wafanyakazi 700 kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi, wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuboresha huduma na kuchochea ongezeko la watalii nchini.

Naye, Mshiriki kutoka Hoteli na Ngorongoro Serena, Faustine Kafunja, amesema “Elimu aliyoipata ataifikisha kwa wafanyakazi wenzake ili kuboresha huduma na wageni kupata huduma zenye viwango stahiki.”

Aidha; watoa huduma hao wamebainisha kuwa Huduma bora watakazopata wageni zitatangaza hoteli na Taifa ili kupata wageni wengi zaidi.

Kadhalika, Meneja wa Chakula na Vinywaji kutoka hoteli ya Parase, Ruben Masaga, amepongeza serikali kwa kuwapatia fursa hiyo ili kukuza sekta ya utalii kwa kutoa huduma bora kwa Mmoja wa wanufaika Anna Benedict kutoka kampuni ya Elewana, amesema mafunzo hayo yamempa ujuzi wa kutoa huduma bora itakayo wavutia watalii.

“Mafunzo haya yatatuondoa kufanya kazi kwa mazoea na kupanua upeo wetu, tunaomba serikali itoe mafunzo haya hata mara tatu kwa mwaka ili ifikapo mwaka 2025 tufikie lengo la serikali la kuwa na watalii wengi,”amesema.

About the author

mzalendoeditor