Featured Kitaifa

MBUNGE NG’WASI AMWAGA PIKIPIKI KWA VIJANA MWANZA

Written by mzalendoeditor

MBUNGE wa Vijana Ng’wasi Damasi Kamani Julai 23, 2023, amekabidhi pikipiki kwa Wilaya zote 7 za Mkoa wa Mwanza ikiwa ni sehemu ya mradi kwa vijana kujiwezesha na kujiinua kiuchumi.

Mbunge Ng’wasi amefanya hivyo ikiwa ni kuunga mkono azma ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapunduzi (UVCCM), Mkoa wa Mwanza kuwajengea uwezo vijana wa Mkoa huo kujiendeleza wenyewe badala ya kukaa mtaani bila kujishughulisha.

About the author

mzalendoeditor